Wakizungumza kwenye kikao cha wamiliki wa pikipiki na madereva Bodaboda,wamesema askari wa Doria wanaotumia Pikipiki ni kero kubwa kwao na kutaka hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.
Wakijibu malalamiko hayo,Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tabora Samwel Mwampashe na Msimamizi wa makosa ya usalama barabarani Mkaguzi Swalehe Digega wamesema Jeshi la Polisi lipo kwa lengo la kusimamia Sheria na sio kupotosha kwani wapo baadhi ya madereva sio waaminifu na kuwataka kutii sheria bila shuruti
Naye Mkuu wa wilaya ya Tabora,Bw.Suleiman Kumchaya amekubali maombi ya waendesha Bodaboda hao kupata elimu kuhusu usalama barabarani ili kupunguza ajali na kuwapunguzia kazi askari wa usalama barabarani.
Kwa mujibu wa Afisa usalama barabarani wilaya ya Tabora,Swalehe Digega, madereva wa bodaboda manispaa ya Tabora hawazingatii sheria za usalama barabarani hivyo husababisha ajali kati ya tatu hadi tano
0 comments: