ABIRIA zaidi ya 5,000 na magari madogo na makubwa 100 waliyokuwa wakisafiri kwenda mikoa ya kaskazin na waliokuwa wakija jijini Dar esalaama na Morogoro wamekwama kwa zaidi ya saa tatu leo Desemba mbili katika barabara kuu ya Chalinze Segera eneo la mto Wami wilayani Bagamoyo mkoani Pwani baada ya njia kufunga.

Katika tukio hilo moja kontena moja na Benzi liliangukia barabarani na hivyo kusababisha magari mengine yanayotumia njia hiyo kushindwa kupita kuendelea na safari hatua ambayo ilileta adha kubwa kwa abiria hasa wa mabasi waliokuwa wakienda mikoa ya Tangam Kilimanjaro,Arusha na Kenya , Daresalaam, Chalinze na Morogoro.
Diwani wa kata ya Mbwewe Madaraka Mbonde amedhibitisha kutokea adha hiyo ambapo amesema alifika eneo la tukio na kukuta maloro hayo yameanguka na hivyo kwa kushirikiana na askari polisi walibuni njia mbadala ya kuyawezesha magari mengine kupita na hivyo kulazimika kutengeneza njia ya vumbi pembezoni (daiveshen) mwa barabara kuu eneo la tukio ili kuyawezesha magari madogo na mabasi kuendelea na safari.
Amesema ubunifu huo uliwezesha zoezi la msururu wa magari kupita japo kwa tabu huku lori lililoanguka likisubir krein kuja kulinyanyua.
Mkuu wa usalama barabarani mkoani Pwani Nassor Sisiwaya amethibitsiha tukio hilo huku akitaja majeruhi wa ajali hiyo ni Mohamed Rashid (35) mkazi wa Tanga na kwamba hali yake inaendelea vema.
Amesema Chanzo cha tukio hilo ni magari hayo mawili kufeli breki kisha kuanza kurudi nyuma na kuanguka na kuziba barabara eneo hilo la Wami.
0 comments: