Pasipoti ni hati inayotolewa na serikali ya nchi kuthibitisha kwamba anayeimiliki ni raia wake kwa madhumuni ya kusafiria katika nchi za nje na ikiomba atambuliwe kama raia wake.
Serikali ya Tanzania inatoa aina tofauti tofauti za pasipoti kwa raia wake kutokana na sheria yake ya mwaka 2002 na utekelezaji wake wa mwaka 2004.
Chombo pekee kilichopewa mamlaka ya kusimamia zoezi la utoaji wa pasipoti ni Idara ya Uhamiaji Tanzania chini ya kamishna mkuu wa uhamiaji.
Mpaka sasa Pasipoti zinapigwa chapa katika makao makuu ya ofisi za Idara ya uhamiaji Dar es salaam na Zanzibar.
Hebu sasa tuzitupie macho aina hizo tofauti za pasipoti zinazotolewa Tanzania:
1.PASIPOTI ZA KAWAIDA(ORDINARY PASSPORTS):
Pasipoti
hii anaweza kupewa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
madhumuni ya kusafiria nje ya Jamhuri ya Tanzania.
2.PASIPOTI ZA HUDUMA(SERVICE PASSPORTS):
Pasipoti hii hutolewa kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayefanya huduma za jamii.
3.PASIPOTI ZA KIDIPLOMASIA(DIPLOMATIC PASSPORTS):
Pasipoti hii hutolewa kwa raia ambaye amepewa haki maalumu ya kupewa pasipoti hiyo na sheria ya mwaka 2002.
4.PASIPOTI ZA AFRIKA MASHARIKI(EAST AFRICAN PASSPORTS):
Pasipoti
hii hutolewa kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye nia ya
kusafiri katika nchi za umoja wa Afrika mashariki.
5.HATI YA KUSAFIRIA YA DHARURA(EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT):
Hati
hii hutolewa kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ana
safari ya dharura lakini hajakamilisha taratibu za kupata pasipoti.
Wakati
mwengine hutolewa kwa raia anayetaka kusafiri nchi za nje na hawezi
kupata pasipoti katika muda muafaka au anayerudishwa kwao kutoka nchi za
nje.
6.CHETI CHA UTAMBULISHO(CERTIFICATE OF IDENTIFY):
Inaweza kutolewa hata kwa mtu asiye raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtu
huyu ambaye hawezi kupata pasipoti kutoka katika nchi ambayo yeye ni
raia au ambaye hana uraia wa nchi yoyote kwa madhumini ya kusafiri nje
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
7.HATI YA KUSAFIRIA YA MKUTANO WA GENEVA(GENEVA CONVECTION TRAVEL DOCUMENT):
Hati hii hutolewa kwa mkimbizi aliyepewa hifadhi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sasa hebu tuangalie vitu gani vinavyohitajika wakati wa kutuma maombi ya kuomba pasipoti ya Tanzania:
1.Cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo au cheti cha uasilia wa muombaji(Iwapo muombaji ana uraia wa kuzaliwa).
2.Cheti cha kuzaliwa cha mzazi au hati ya kiapo ya mzazi au cheti cha uasilia wa mzazi(Iwapo mzazi ana urai wa kuzaliwa).
3.Picha za pasipoti za hivi karibuni zinazokuonyesha vizuri na kama zitakavyoainishwa na mamlaka husika.
4.Kwa suala kama la muombaji kuwa chini ya umri wa maika 18, mzazi au mlezi ataandika makubaliano.
ZINGATIA:
Hati ya kiapo ya kuzaliwa ya muombaji inatakiwa iapwe na:
*Mzazi au mlezi wa kisheria;
*Mtu aliyeshuhudia kuzaliwa kwa muombaji wa pasipoti na ambaye anamzidi muombaji si chini ya miaka 5;
*Ndugu wa karibu wa muombaji ambaye alitaarifiwa kuzaliwa kwa muombaji na wazazi wake.
Kuna kipindi Kamishna mkuu wa uhamiaji anaweza akamtaka muombaji athibitishe uraia wa wazazi wake.
SASA UMESHAYAJUA MAHITAJI YA KUPATA PASIPOTI, JIPANGE NA TAARIFA HIZO ILI UNAPOHITAJI USIPATE USUMBUFU.
It would have been more friendly if guidance could be given before filing up the forms. I filled the form and upon submission that's when I got asked to provide a number which from the beginning it was not indicated as a pre-requisite. Now I don't know how to get the number. It means I have to fill the same all over again.
ReplyDeleteAsante nimekupata vizuri kuhusu hio hati ya kusafiria
ReplyDeleteJe,ni hatua gani za kufuata ili kupata hio paspoti ya kawaida(ORDINARY PASSPORT)?
ReplyDeleteJe,ni kuanzia miaka mingapi (umri) wa mtu unaweza kupata passpoti? Pia hatua zipi za kuomba passport kwa mtoto wa umri wa miaka 4?
ReplyDeleteHii ndiyo Tanzania...
ReplyDelete