Kuogelea ni sehemu mojawapo
ya burudani kwa walio wengi hasa wale wanaoishi katika maeneo yenye fukwe za
bahari, maziwa na hata mito.
Kama wewe ni mmoja
wao na unampango wa kutembelea mkoa wa Morogoro unaweza kupata changamoto
kidogo maana mji huo kama unavyojulikana ni mji kasoro bahari, hauna bahari
hivyo swala la kuogelea linaweza kuwa issue.
Japo bwawa la mindu
lipo lakini hairuhusiwi kuogelea humo maana ni hatari na inatajwa kuwa ni
uchafuzi wa maji ambayo hutumika na mamlaka ya maji mkoani humo.
Oasis Hotel
Hata hivyo kwa kujali
mahitaji ya watu wengi kutaka maeneo ya kuogelea kuna hoteli tatu zimejenga
mabwawa ya kuogelea nazo ni Nashera Hotel, Morogoro Hotel na Oasis Hotel ambazo
zote ziko Morogoro mjini.
Nashera Hotel
Kama utachukua chumba
cha hoteli katika moja ya hoteli hizo basi unaweza kuogelea bila kulipa
chochote lakini kwa wale ambao wanapenda kwenda kuogelea tu gharama zake ni sh.
5000 pesa ya kitanzania.
0 comments: