Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich
Matei alisema dereva huyo aliyekuwa alikitoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo (DRC), alikutwa na mauti hayo akiwa ndani ya gari aina ya Leyland
Daf alilokuwa akiendesha kuelekea Dar es Salaam.
Kamanda Matei alisema kabla ya dereva
huyo mwenyeji wa Mkoa wa Iringa kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa
akilalamika kuwa anajisikia vibaya walipokuwa njiani.
Akizungumzia tukio hilo utingo wa lori
hilo, Said Hemed (22) alisema: “Tulianza safari vyema, lakini
tulipokaribia Chalinze, akaanza kulalamika kuwa hajisikii vizuri.
Tuliendelea na safari, huku nampa moyo lakini alirudia maneno hayo
tulipofika Mlandizi, lakini alikuwa akinieleza itambidi kwenda kupima
pindi akifika tu Dar es Salaam.
“Tukaendelea na safari na jamaa alikua
safi tu akiendesha, lakini tulipokuwa kati ya Mlandizi na Kibaha
alirudia kusema mwili wake kama haupo vizuri vile na tulipokuwa katikati
ya safari kabla ya kufika Misugusugu aliniambia... ‘Dogo hali siyo
nzuri ninaumwa aisee’.
“Nikamuuliza sasa kuendesha utaweza
kweli? Akaniambia Mungu ni mwema, nitajitahidi tufike Dar es Salaam ili
nikafanye vipimo kabisa maana hali siyo nzuri. Tukaja hadi hapa check
point (kituo cha ukaguzi) sasa akawa ananieleza huku kalalia usukani.
Mimi nikateremka kuangalia kinachoendelea, kwani ilikuwa foleni ndefu
kiasi. Muda mfupi nikarudi kwenye gari, kufika nikamkuta ‘bro’
amefariki, yaani ni kama kaniambia hebu nipishe naondoka. Sikuamini
lakini ndivyo ilivyotokea.”
Kamanda Matei alisema kuwa mwili wa
marehemu ulichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya
kuhifadhiwa pamoja na kufanyiwa uchunguzi.
Ofisa Habari wa Hospitali ya Tumbi, Gerald Chami alisema vipimo vilichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi.
Hemed alisema baadaye kuwa baada ya
tukio hilo alifanya utaratibu wa kuliingiza lori hilo katika yadi ya
magari iliyopo eneo hilo na baadaye kufanya mawasiliano na tajiri yake
kwa ajili ya utaratibu wa kuuhifadhi mwili pamoja na gari.
Na Julieth Ngarabali
0 comments: