News Alert: Meli ndogo ya mizigo yazama kilwa masoko, mtu mmoja hajulikani aliko



Na Abdulaziz Video, Kilwa 
Mtu mmoja aliefahamika kwa Jina la Nice Mtega fundi mkuu wa Meli ndogo ya mizigo iitwayo MV MERCI II inayomilikiwa na Semuhungu Shingiro anahofiwa kufa maji baada ya kutoweka kwa zaidi ya masaa 36 toka kuzama kwa meli hiyo katika bandari ya Kilwa masoko.
 Akiongea na Globu ya Jamii hii iliyofika katika eneo hilo, meneja wa Bandari ya Kilwa, Bw. Iddi Omary,  alieleza kuwa Meli hiyo iliyofunga gati jana jioni ikitokea songosongo na  kupakia tani 30 za mchanga na tani 30 za maji ilizama majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo ambapo Nahodha wa Meli hiyo Captain Charles Kalinga na wasaidizi wake 3 walifanikiwa kutoka ila Nice Mtega aliekuwepo ndani hajaonekana hadi sasa. Juhudi za kumtafuta na kuinua meli hiyo zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado hazijajulikana
Meli hiyo ikiwa imezama majini katika gati la Kilwa Masoko
Sehemu ya chini ya meli

MERCI III kabla ya kuzama
Meli ikiwa majini

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: