Majina haya ya mabasi yaendayo kusini yanamaanisha nini?

Mtandao wa mpini wa shoka katika moja ya safari zake kati ya Dar-Mtwara-Dar, ulifanikiwa kukusanya majina ya mabasi yanayokwenda kwenye mikoa hiyo.


Sehemu kubwa ya majina ya mabasi yanayokwenda (yanayopita) kusini, yanafurahisha kwa namna yake. tazama picha uone majina yenyewe.

Hili Linaitwa Somea. Sasa sijui linakuhimiza usomee kitu gani hasa! Hili linaitwa Wifi. Sasa sijui ni wifi yake nani! Na mimi nikianzisha basi langu nitaliita Shemeji Au Shangazi. Unaonaje hiyo!

Hili linaitwa Karafuu. Sijui ni karafu za Zenji (Zanzibar), au ni za wapi yakhe! Mimi basi langu nitalipa jina la Kitunguu Trans Au Ngogwe Trans (Nyanya chungu).  Hili linaitwa Mkuu. Sasa sijui ni Mkuu wa Meza..! Mkuu wa Majeshi..! Mkuu wa nchi..! Au mwenye basi hili asilia yake hasa ni kutoka eneo la Mkuu-wilaya ya Rombo, mkoa wa Kilimanjaro!  Hili linaitwa Najma (soma ubavuni). Yawezekana ni jina la binti wa mwenye basi, Au ni la mke wake mdogo, kipenzi cha roho!


 Hili linaitwa Siri Yako. Sijui hata ni siri ya kitu gani iliyomo ndani ya basi hili!

Hapa ni Swahili. Ndani ya hili basi yawezekana ni marufuku kuzungumza lugha nyingine yoyote ile. Ni Kiswahili tu pekee ndicho kinachoruhusiwa. Haiwezekani! Je kama Wakorea, Wachechnya, Waalbania na Waturuki wasiojua kabisa kiswahili wakitaka kusafiri na basi hili, ina maana itawabidi wao wawe kama mabubu tu mwanzo wa safari hadi Mwisho!

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: