Mkurugenzi wa Sumatra CCC, Oscar Kikoyo, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana na kusema kuwa kutokana na wingi wa abiria kuna baadhi ya watoa huduma wasio waaminifu hupandisha nauli bila kufuata kanuni.
Kikoyo alisema ni vema abiria kuwa na tabia ya kushirikiana na mamlaka zilizopewa jukumu kuhakikisha wanasafiri kwa usalama ili kukomesha vitendo vinavyohatarisha usalama na maisha yao.
Alisema usalama wa abiria ni muhimu kuliko safari yenyewe, hivyo ni wajibu wao kutoa taarifa bila woga wala kuhofia, ili kuepukana na vitendo vya ulaghai, kuuziwa tiketi za safari kwa bei juu, kupandishwa kwenye basi bovu na kubadilishiwa basi alilopangiwa kusafiri nalo.
Baraza hilo pia limewataka abiria wanaotumia usafiri wa treni inayotoa huduma kati ya Stesheni na Ubungo Maziwa na lile la Tazara–Mwakanga kuacha tabia ya kudandia pindi treni linapoanza safari.
0 comments: