PICHA::Abiria wa Dalala Wanusurika ‘Kifo’ Gongo la Mboto

Gari hilo pichani likiwa limetumbukia kwenye mitaro ya pembeni mwa barabara eneo la Gongo la Mboto na askari wa usalama barabarani wakijitahidi kuyaondoa magari yaliyogogwa na gari hilo, huku baadhi ya wananchi wakishuhudia.

ABIRIA wa daladala moja namba T608 BKP aina ya Toyota Hiace eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam leo wamenusurika kifo baada ya gari hiyo iliyokuwa ikielekea Moshi-Baa kupata ajali ikiwa inawakimbia wafanyakazi wa SUMATRA, ajali hiyo imetokea leo majira ya jioni baada wa dereva wa daladala hiyo kuona gari la Sumatra na kuanza kutimua mbio bila kujali usalama wa abiria.
Dereva huyo aliyekuwa anatumia barabara za pembezoni mwa barabara kuu alianza kuendesha gari hilo kwa kasi na baada ya askari kumuona walimfuata na kumzuia ili wamuhoji baada ya kuzuiwa kwa mbele gafla aliondoa gari kwa kasi na kuingia uchochoro mwingine kisha kutaka kuingia barabara kubwa kwa kasi ndipo alipogogana na gari lingine dogo lililokuwa likipita.
Kama vile mchezo wa kuigiza wa mbio za magari dereva huyo aliwasha tena gari hilo likiwa tayari limeumia na kutaka kukimbia kwa kasi ndipo lilipomshinda na hatimaye kuingia mtaroni na kukwama. Ghafla dereva huyo alishuka kwenye gari na kuanza kutimka lakini askari na baadhi ya wananchi walimtia mikononi baada ya hatua chache ndipo wananchi wenye hasira wakaanza kumpiga hadi walipo zibitiwa na askari waliofika eneo la tukio hilo muda mfupi.
Abiria walianza kujinusuru kwa kutoka ndani ya gari hilo wakikimbia huku wengine wakitokea madirishani. Hata hivyo mmoja wa abiria alizimia kutokana na tukio hilo hivyo kukimbizwa hospitalini kwa msaada zaidi. Baadhi ya mashuhuda waliozungumza na mtandao huu walisema dereva huyo alikuwa akiwakimbia Sumatra kwani daladala hiyo ilikuwa ni bubu hivyo alihofia kukamatwa ndipo alipoanza kutimua mbio hovyo. Hata hivyo hakuna abiria aliye jeruhiwa kwa ajali zote mbili zilizotokea wakati gari hilo likitimua mbio.Credit: The Habari.com

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: