TAZAMA HATARI YA BARABARA YA NDADA KUELEKEA MASASI MKOANI MTWARA

Magari yakipishana kwa shida katika eneo hilo la Kijiji cha Mkalapa,Mkoani Mtwara kutokana na kuharibika kwa barabara hiyo.
Wakazi wa kijiji hicho pamoja na Abiria wanaosafiri kwenda Newala,Masasi,Nachingwea,Nanyumbu na Tunduru wakiwa wamesimama bila kujua cha kufanya wakati magari yakiwa yamekwama.
*******
Na Abdulaziz Video,Masasi.

Barabara ya Ndanda kwenda Masasi eneo la Kijiji cha Mkalapa,limekuwa ni majanga matupu kama inavyoonekana katika picha hapo chini,kwani barabara hiyo imeharibika vibara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha matika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Abiria wanaofanya safari katika maeneo hayo,inapaswa wajiandae kwa kupoteza masaa kadhaa katika eneo hilo,kwani mambo hayajakaa sawa.

Hivyo wakala wa Barabara Mkoa wa Mtwara (TANROADS),wanapaswa kulishughulikia swala hili haraka iwezekanavyo ili kuwaepusha watumiaji wa barabara hiyo kuondokana na hadha hii inayowaathiri wasafiri waendao Newala,Masasi,Nachingwea,Nanyumbu na Tunduru.

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: