Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mombasa hadi Nairobi hatimaye
utaendelea, baada ya kutiwa saini makubaliano ya ufadhili kati ya
serikali ya Uchina na Kenya. Reli hiyo itakayoendelezwa hadi Kigali na
Juba imenuiwa kuunganisha mataifa ya 7 ya eneo la Afrika Mashariki
yakiwemo Kenya, Uganda,Tanzania,
Rwanda, Burundi, Sudan Kusini na Ethiopia. Kenya ambayo imepata
ufadhili wa asilimia 90 ya sehemu yake ya mradi huo Utagharimu kiasi cha
Dola bilioni 3.7 itawasilisha leo mchango wake wa asilimia kumi kwa
serikali ya China.
chanzo DW (J M)
0 comments: