#DerevaMakini: Wajibu wa taasisi, makampuni katika kupunguza ajali za mabasi ya abiria (1)


Nawasalimu nyote kwa jina la uzalendo na utaifa uliotukuka, leo katika mwendelezo wa kampeni ya #DerevaMakini ambayo inalenga kuishirikisha jamii katika kukabiliana na ajali ambazo zimekuwa mwiba kwa taifa, nitaangazia wajibu wa taasisi, makampuni na watu binafsi katika kupunguza ajali hizo.

Katika makala ya awali nilitaja orodha ndefu ya wadau wanaohusika moja kwa moja kwenye sekta ya usafiri ambao wakitekeleza sawasawa majukumu yao ajali zinaweza kupungua kama sio kukoma kabisa. Hivyo leo nitaanza na makampuni ya simu za mkononi.

Mchango wa makampuni ya simu za mkononi katika maendeleo ya sekta ya mawasiliano na uchumi kwa taifa ni mkubwa sana, lakini pamoja na manufaa hayo bado kuna madhara makubwa yanayotokana na matumizi mabaya ya simu za mkononi kwa madereva wakati wakiendesha magari yao.

Kwa mujibu wa Mtandao wa DailyMaily, takwimu zinaonyesha kuwa Dereva mmoja (1) kati ya wanne (4) wanaotumia simu zao za mkononi huku wakiendesha magari yao hupata ajali zenye ukubwa na madhara mbalimbali.

Hapa ndio swali langu linapoibuka; Je, Makampuni ya simu zamikononi yamejiwekea mikakati gani kuelimisha wateja wake juu ya madhara ya matumizi ya simu wakati wakiendesha? Au wanachojali wao ni kutengeneza faida tu pasipo kuangalia madhara yanayowakumba wateja wao?

Tumeona ushiriki wa baadhi ya makampuni hayo katika wiki za nenda kwa usalama yakihimiza usalama barabarani, lakini ingefaa zaidi kama ushiriki wao ungekuwa endelevu, pengine wangeweka hata jumbe kwenye kadi za muda wa maongezi ili kila anayenunua muda huo aweza kupata elimu Fulani.

Sote ni mashahidi kwa makampuni yanayouza vileo, sheria inayalazimisha kuweka onyo juu yamadhara yanayoweza kumpata mtumiaji endapo atatumia bidhaa hizo vibaya, jambo ambalo  linawezwa kuigwa na makampuni ya simu nayo yakaanza kutoa onyo la matumizi mabaya ya simu kwa madereva wanapoendesha.

Ni mtazamo tu, na wewe msomaji kupitia forum hii unaweza kutupia mawazo, mtazamo, ushauri na hata maswali yako ukizingatia mada aliyetajwa hapo juu, maoni yako tutayatumia kwenye mada ifuatayo.

Wiki ijayo tutaendelea kuwaangalia wadau wengine na majukumu yao wakiwemo Askari wa Usalama Barabarani, Madereva, Abiria, Wamiliki wa vyombo vya usafiri, Sumatra, Vyombo vya habari, Tanroads, Miundombinu , TBS, Wauzaji wa magari, Sheli za mafuta na vipuli vya magari. 

Kampeni hii ya #DerevaMakini inayolenga kupunguza ajali za barabarani ikijikita zaidi kwenye mabasi ya abiria imewezeshwa na Michuzi Blog, Tabianchi Blog na Transevents Marketing

Kwa taarifa zaidi tembelea Dereva Makini
read more →

KITUO CHA DALADALA MWENGE KUFUNGWA RASMI JUMAPILI HII


Wamiliki, madereva na abiria wote mnatangaziwa kuwa kituo cha daladala Mwenge kitafungwa rasmi siku ya Jumapili jioni tarehe 01.06.2014. Kuanzia siku ya jumatatu asubuhi tarehe 02.06.2014 kituo kitakachokuwa kinatumika ni Makumbusho tu.
Sababu kubwa ya kufunga kituo hicho ni ufinyu wa eneo hilo jambo linalochangia dadalada kushindwa kuingia kituoni kwa wakati hasa vipindi vya asubuhi na jioni hivyo kusababaisha foleni kubwa katika eneo la Mwenge.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa eneo hilo kwa sasa litabaki kuwa eneo la wazi.

Madereva mnatakiwa kutii agizo hili ili kuepukana na hatua kali ambazo zitachukuliwa dhidi ya yeyote ambae atakaidi, aidha abiria mnatakiwa msilazimishe kushushwa eneo ambalo hakuna kituo cha daladala.

Barabara za kuingia na kutoka kituoni Makumbusho zinaendelea kukarabatiwa na Manispaa ya Kinondoni ili kusiwe na tatizo la kuingia kituoni hapo.

Conrad Shio
Afisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki

Wamiliki, madereva na abiria wote mnatangaziwa kuwa kituo cha daladala Mwenge kitafungwa rasmi siku ya Jumapili jioni tarehe 01.06.2014. Kuanzia siku ya jumatatu asubuhi tarehe 02.06.2014 kituo kitakachokuwa kinatumika ni Makumbusho tu.
Sababu kubwa ya kufunga kituo hicho ni ufinyu wa eneo hilo jambo linalochangia dadalada kushindwa kuingia kituoni kwa wakati hasa vipindi vya asubuhi na jioni hivyo kusababaisha foleni kubwa katika eneo la Mwenge.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa eneo hilo kwa sasa litabaki kuwa eneo la wazi.

Madereva mnatakiwa kutii agizo hili ili kuepukana na hatua kali ambazo zitachukuliwa dhidi ya yeyote ambae atakaidi, aidha abiria mnatakiwa msilazimishe kushushwa eneo ambalo hakuna kituo cha daladala.

Barabara za kuingia na kutoka kituoni Makumbusho zinaendelea kukarabatiwa na Manispaa ya Kinondoni ili kusiwe na tatizo la kuingia kituoni hapo.

Conrad Shio
Afisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki
read more →

MRADI WA UJENZI WA RELI KUTOKA MOMBASA - DAR ES SALAAM


Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mombasa hadi Nairobi hatimaye utaendelea, baada ya kutiwa saini makubaliano ya ufadhili kati ya serikali ya Uchina na Kenya. Reli hiyo itakayoendelezwa hadi Kigali na Juba imenuiwa kuunganisha mataifa ya 7 ya eneo la Afrika Mashariki yakiwemo Kenya, Uganda,Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini na Ethiopia. Kenya ambayo imepata ufadhili wa asilimia 90 ya sehemu yake ya mradi huo Utagharimu kiasi cha Dola bilioni 3.7 itawasilisha leo mchango wake wa asilimia kumi kwa serikali ya China.
chanzo DW (J M)
read more →

KUHUSU DEREVA ALIYEFARIKI DUNIA AKIWA KWENYE FOLENI YA UKAGUZI JIJINI DAR ES SALAAM


Dereva wa malori ya safari za masafa marefu Charles Mbungu (46), amefariki dunia akiwa ndani ya lori alipokuwa katika foleni ya ukaguzi wa magari kwenye Kituo cha Misugusugu, Kibaha, Pwani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema dereva huyo aliyekuwa alikitoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), alikutwa na mauti hayo akiwa ndani ya gari aina ya Leyland Daf alilokuwa akiendesha kuelekea Dar es Salaam.
Kamanda Matei alisema kabla ya dereva huyo mwenyeji wa Mkoa wa Iringa kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa akilalamika kuwa anajisikia vibaya walipokuwa njiani.
Akizungumzia tukio hilo utingo wa lori hilo, Said Hemed (22) alisema: “Tulianza safari vyema, lakini tulipokaribia Chalinze, akaanza kulalamika kuwa hajisikii vizuri. Tuliendelea na safari, huku nampa moyo lakini alirudia maneno hayo tulipofika Mlandizi, lakini alikuwa akinieleza itambidi kwenda kupima pindi akifika tu Dar es Salaam.
“Tukaendelea na safari na jamaa alikua safi tu akiendesha, lakini tulipokuwa kati ya Mlandizi na Kibaha alirudia kusema mwili wake kama haupo vizuri vile na tulipokuwa katikati ya safari kabla ya kufika Misugusugu aliniambia... ‘Dogo hali siyo nzuri ninaumwa aisee’.
“Nikamuuliza sasa kuendesha utaweza kweli? Akaniambia Mungu ni mwema, nitajitahidi tufike Dar es Salaam ili nikafanye vipimo kabisa maana hali siyo nzuri. Tukaja hadi hapa check point (kituo cha ukaguzi) sasa akawa ananieleza huku kalalia usukani. Mimi nikateremka kuangalia kinachoendelea, kwani ilikuwa foleni ndefu kiasi. Muda mfupi nikarudi kwenye gari, kufika nikamkuta ‘bro’ amefariki, yaani ni kama kaniambia hebu nipishe naondoka. Sikuamini lakini ndivyo ilivyotokea.”
Kamanda Matei alisema kuwa mwili wa marehemu ulichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya kuhifadhiwa pamoja na kufanyiwa uchunguzi.
Ofisa Habari wa Hospitali ya Tumbi, Gerald Chami alisema vipimo vilichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi.
Hemed alisema baadaye kuwa baada ya tukio hilo alifanya utaratibu wa kuliingiza lori hilo katika yadi ya magari iliyopo eneo hilo na baadaye kufanya mawasiliano na tajiri yake kwa ajili ya utaratibu wa kuuhifadhi mwili pamoja na gari.
Na Julieth Ngarabali
read more →

ZIFAHAMU HOTELI ZENYE SWIMMING POOL MKOANI MOROGORO


Kuogelea ni sehemu mojawapo ya burudani kwa walio wengi hasa wale wanaoishi katika maeneo yenye fukwe za bahari, maziwa na hata mito.

Kama wewe ni mmoja wao na unampango wa kutembelea mkoa wa Morogoro unaweza kupata changamoto kidogo maana mji huo kama unavyojulikana ni mji kasoro bahari, hauna bahari hivyo swala la kuogelea linaweza kuwa issue.

Japo bwawa la mindu lipo lakini hairuhusiwi kuogelea humo maana ni hatari na inatajwa kuwa ni uchafuzi wa maji ambayo hutumika na mamlaka ya maji mkoani humo.

 Morogoro Hotel
 Oasis Hotel
Hata hivyo kwa kujali mahitaji ya watu wengi kutaka maeneo ya kuogelea kuna hoteli tatu zimejenga mabwawa ya kuogelea nazo ni Nashera Hotel, Morogoro Hotel na Oasis Hotel ambazo zote ziko Morogoro mjini.

Nashera Hotel
Kama utachukua chumba cha hoteli katika moja ya hoteli hizo basi unaweza kuogelea bila kulipa chochote lakini kwa wale ambao wanapenda kwenda kuogelea tu gharama zake ni sh. 5000 pesa ya kitanzania.
read more →

Dondoo: Mahitaji muhimu ya kuambatanisha wakati wa kuomba pasipoti/hati ya kusafiria

Kipindi kilichopita tuliona aina za pasipoti zinazotolewa nchini Tanzania na baadhi ya taarifa unazotakiwa kuwa nazo ili uweze kuipata.

Leo tutaangalia hati zitazokusaidia pia upate pasipoti kwa urahisi endapo utaambatanisha katika maombi yako kutokana na aina ya safari unayotaka kufanya:

1.SAFARI BINAFSI
Maombi yako unatakiwa uambatanishe na:
*Ushahidi wa shughuli unayofanya;
*Barua ya mualiko;
*Tiketi ya kurudi;
*Barua ya ruhusa ya mzazi kama muombaji yuko chini ya miaka 18;
*Barua ya ruhusa kutoka kwa muajiri wako kama umeajiriwa;
*Barua kutoka kwa mjumbe wa eneo unalokaa muombaji.

2.SAFARI YA AJIRA
Unatakiwa uambatanishe na:
*Tangazo la kazi;
*Tiketi ya kurudi;
*Barua kutoka kwa mjumbe wa eneo unaloishi.

3.SAFARI YA KIMASOMO
Maombi yako yaambatane na:
*Barua ya kuchaguliwa na shule/chuo;
*Vyeti vyako vya masomo;
*Barua ya udhamini;
*Ushahidi wa malipo kama unajilipia binafsi;
*Barua ya ruhusa kutoka kwa muajiri wako kama umeajiriwa;
*Barua ya ruhusa kutoka kwa mzazi kama una umri chini ya miaka 18.

4.SAFARI YA KIDINI
Maombi yako yanatakiwa yaambatane na:
*Barua ya mualiko;
*Barua kutoka katika taasisi ya dini iliyoandaa safari.

5.SAFARI YA KIMATIBABU
Maombi yako yaambatane na:
*Barua kutoka kwa mganga mkuu;
*Ushahidi wa barua kutoka kwa daktari aliyekuwa anakutibu;
*Barua kutoka wizara ya Afya.

6.SAFARI YA KIMICHEZO
*Barua kutoka shirikisho la mpira TFF au ZFA;
*Barua kutoka katika chama cha michezo kilichosajiliwa;
*Barua ya kualikwa.

7.SAFARI YA SKAUTI
Maombi yanatakiwa yaambatanishwe na:
*Barua kutoka kwa chama husika cha skauti;
*Barua ya ruhusa kutoka kwa mzazi kama una umri chini ya miaka 18;
*Barua ya mualiko.

8.SAFARI YA KIKAZI
Maombi yako yaambatane na:
*Barua kutoka kwa muajiri;
*Barua ya mualiko;
*Kitambulisho chako.

9.SAFARI YA KIBIASHARA
Maombi yako yanatakiwa yaambatanishwe na:
*Leseni halali ya biashara;
*Tiketi ya kurudi.

10.SAFARI YA UBAHARIA
Maombi yako yanatakiwa yaambatane na:
*Mkataba wa ajira;
*Vyeti vya taaluma;
*Barua kutoka kwa umoja wa mabaharia.

MAHITAJI YANAYOTAKIWA ILI UPATE HATI YA KUSAFIRIA:

1.HATI YA KUSAFIRIA YA DHARURA
Maombi yako yanatakiwa yaambatane na:
*Picha nne ndogo za pasipoti

2.CHETI CHA UTAMBULISHO
Muombaji wa cheti cha utambulisho anatakiwa awe na:
*Ripoti maalumu ya polisi ikiwa hakuna ubalozi;
*Picha mbili za pasipoti.

3.HATI YA KUSAFIRIA YA AGANO LA GENEVA
Muombaji wa hati hii anatakiwa awe na:
*Barua kutoka kwa mkurugenzi anayesimamia idara ya wakimbizi;
*Nakala ya kitambulisho cha ukimbizi;
*Picha mbili za pasipoti.

MAOMBI YA KUBADILISHIWA PASIPOTI NA HATI ZA KUSAFIRIA ZILIZOHARIBIKA:

Ikiwa pasipoti au hati yako ya kusafiria imeharibika kabisa au 
iko katika hali ambayo ni 
lazima ibadilishwe, 
muombaji anatakiwa 
atume maombi kwenda kwa 
kamishna wa huduma za uhamiaji.

1.KUBADILISHIWA PASIPOTI
Muombaji anatakiwa awe na:
*Pasipoti iliyoharibika;
*Picha nne za pasipoti.

2.KUBADILISHIWA HATI YA KUSAFIRIA
Muombaji anatakiwa awe na:
*Hati za kusafiria zilizoharibika;
*Picha mbili za pasipoti.

MAOMBI YA KUTENGENEZEWA PASIPOTI MPYA KWA ILIYOPOTEA AU KUIBWA:

Ikiwa pasipoti imepotea au kuibiwa maombi ya kutengenezewa mpya 
yanatakiwa yaambatane 
na kiapo pamoja 
ripoti ya mamlaka ambayo
 muombaji alitoa taarifa ya kupotelewa au kuibiwa.

Muombaji anatakiwa awe na:
*Ripoti kutoka katika kituo cha polisi alichopeleka taarifa ya kuibiwa;
*Taarifa uliyotoa kupotelewa na pasipoti katika gazeti la kila siku.

KUBATILISHWA PASIPOTI AU HATI YA KUSAFIRIA
Kamishna wa idara ya uhamiaji katika muda wowote ana mamlaka ya 
kubatilisha pasipoti au 
hati ya kusafiria kwa aliyepewa ikiwa aliyenayo amefanya yafuatayo:

*Ameruhusu pasipoti yake itumiwe na mtu mwengine;
*Amefukuzwa nchini na serikali;
*Ikiwa aliyenayo amesitisha uraia wake wa Tanzania;
*Ikiwa aliyenayo amejihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, 
utengenezaji wa hela bandia, kuingiza isivyo halali wahamiaji, 
amejihusisha na ugaidi, 
na hata uhamishaji wa hela kimagendo;
*Ikiwa kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi.

ADA YA MAOMBI YA PASIPOTI NA HATI ZA KUSAFIRIA:
1.Pasipoti ya kawaida-50,000/=

2.Pasipoti ya kidiplomasia-50,000/=

3.Pasipoti ya huduma-50,000/=
read more →