TAARIFA KAMILI YA MTUMBWI ULIOZAMA MTWARA JANA MARCH 13 NA KUUA WATU 3

Taarifa kutoka Mtwara ambazo zimethibitishwa na jeshi la Polisi ni kuhusu Mtumbwi ambao umezama wakati ukivuka kutoka kitongoji cha Ng’wale kwenda ng’ambo ya pili ambapo ndiyo sehemu waliyokuwa wanashukia abiria waliokuwepo.
Tayari watu 21 wamefikishwa katika hospital ya mkoa wa Mtwara kwa matibabu ambao wote ni wakina mama pamoja na mtoto mmoja wa kiume wa mwaka 1 huku waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo wakiwa ni wakina mama 3.
Mtumbwi huo unahisiwa ulikuwa na abiria 24 ambapo pamoja na wahusika wawili wa mtumbwi huo kwa pamoja, jumla ya watu waliokua kwenye mtumbwi ni 26 ambapo Polisi wanasema kina mama hao walikua wanatoka kutafuta samaki kwa ajili ya biashara.
Jeshi la polisi bado linamtafuta aliekua anauendesha huo Mtumbwi ambae inasemekana aliogelea na kutoweka baada ya mtumbwi kuzama.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika ingawa baadhi ya abiria wanadai ni upepo mkali na mvua iliyokuwa inanyesha kwenye eneo hilo

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: