Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
Wakala
wa Mradi wa Mabasi yaendayo aaraka (DART) umesema kabla ya utekelezaji
wa awamu ya kwanza ya mradi kukamilika, mwaka huu kutakuwa na mabasi
machache ambayo yataanza kutoa huduma ya usafiri kutoka Kimara hadi
Kivukoni.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa (DART), Bi. Asteria Mlambo aliwambia waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam hivi karibu kuwa utekelezaji wa awamu ya
kwanza unaendelea vizuri na kabla ya kukamirika hapo mwakani,kutakuwa na
mabasi machache yataanza kufanya kazi mwaka huu.
“Mradi
huu wa mabasi haya unatarajia kukamilika mwaka ujao lakini juhudi
zinafanyika kuhakikisha mwaka huu yanapatikana mabasi machache kuanza
kutoa huduma,”alisema Bi. Mlambo.
Alisema
utekelezaji wa mradi huu umegawanyika katika awamu sita katika jij la
Dar-es-salaam ambapo kwa sasa wapo katika awamu ya kwanza na inaendelea
vizuri.
“Katika
awamu hii ya kwanza wakandarasi wapo katika mafungu makuu sita, ambapo
fungu la kwanza ni ujenzi wa barabara unaofanywa na kampuni ya strabag
ya ujerumani kuanzia Kimara hadi Kivukoni,” alisema.
Fungu
la pili ni kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo ambako kunaajengwa
maegesho na karakana ya mabasi kwa ajili ya kufanyia mabasi matengnezo.
Bi.
Mlambo alisema fungu la tatu ni ujenzi wa kituo cha maegesho eneo la
jangwani ambacho pia kutajengwa makao makuu ya mradi kwa ajili ya
maswala ya kiutawala.
Alisema
fungu la nne ni eneo la kivukoni ambako ujenzi wake umefikia asilimia
90, fungu la tano ni ujenzi kituo kikuu eneo la Kariakoo Gerezani
Quarter na fungu la sita ni vituo vidogo ambavyo vitashusha na kupakia
abiria.
“Vituo
hivi vidogo vitawaunganisha abiria kutoka maeneo wanayoishi na mfumo wa
mabasi haya,”alisema mtendaji mkuu huyo na kuongeza kuwa maendeleo ya
ujenzi wa mradi yanaridhisha.
Akifafanua
zaidi alisema mpaka hivi sasa utekelezaji wa mradi huo upo katika
kiwango cha 55% ya ujenzi wa miundombinu unasimamiwa na Wakala wa
Usimamiaji wa Barabara nchini (TANROADS).
“Kampuni
ya ushauri ya Rebel Group kutoka Uholanzi ambayo ilishanda zabuni
itasaidia kupata watoa huduma baada ya kutangazwa tenda hiyo hapo mwezi
mei, mwaka huu,” alisema.
Alisema
katika utekelezaji mradi huo wakala ulikutana na changamoto mbalimbali
ikiwemo ya kuwepo kwa huduma mbalimbali zilizokuwa zinaendeshwa kando ya
barabara ambapo wakala ulilazimika kuingia gharama kuviondosha.
Wakala
wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka ambao upo chini ya Ofisi ya Waziri
Mkuu Serikali za Mitaa na Tawala za mikoa (TAMISEMI) unatekeleza maradi
wa mabasi hayo ili kutatua kero ya msongamano wa magari katika jiji la
Dar es Salaam.
0 comments: