Mamlaka
ya Udhibiti, Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imesitisha
leseni za usafirishaji kwa mabasi yanayomilikiwa na Kampuni ya Osaka
Royal Class, Polepole Classic na Burhan Bus Service.
Uamuzi huo
umetokana na mabasi ya kampuni hizo, kuhusika kwenye ajali zilizotokea
katika maeneo, siku tofauti ambapo watu walipoteza maisha na wengine
kujeruhiwa.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Meneja
Mawasiliano wa SUMATRA, Bw. David Mziray, alisema Desemba 10 mwaka huu,
basi la Osaka Royal Class lenye namba T819 BYL, lilipata ajali na kuua
watatu na majeruhi 33.
Basi hilo lilikuwa likitoka Arusha kwenda Dar
es Salaam na ajali hiyo ilitokea kwenye eneo la Kirinjiko, Wilaya ya
Same, mkoani Kilimanjaro, ambapo chanzo cha ajali ni dereva wake
kushindwa kulimudu na mwendo kasi.
“Kwa kuzingatia Kifungu namba 15
cha Sheria ya SUMATRA na pia Kanuni namba 22 ya Kanuni za Ufundi,
Usalama na Ubora wa Huduma za mwaka 2008, Mamlaka imeamua kusitisha
leseni za usafirishaji kwa mabasi yanayomilikiwa na kampuni hii.
“Mabasi
hayo ni yenye namba T819BYL, T417 AAG, T852 AUL, T206 CJZ, T201 CJZ,
T437 BJK na T852 AUL, yatapewa leseni za usafirishaji baada ya
kutekeleza maagizo.
Maagizo hayo ni kuhakikisha mabasi ya kampuni
hiyo ambayo namba zake zimetajwa, yakaguliwe na Mkaguzi kutoka Jeshi la
Polisi na kuthibitisha kama yanakidhi viwango vya ufundi na usalama.
Madereva
wa mabasi yaliyotajwa wajaribiwe na Jeshi la Polisi ili kujiridhisha
kama wana sifa za kuendesha mabasi, kuwasilisha kwa maandishi mpango
utakaotumiwa na kampuni kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa
na madereva wake.
Alisema Kampuni ya Polepole Classic, Desemba 8
mwaka huu, basi lenye namba T 898 BKN, lilipata ajali Kijiji cha
Machangarawe, Wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Ajali hiyo
ilisababisha vifo vya watu watano na majeruhi 32 ambapo taarifa za Jeshi
la Polisi zilisema chanzo cha ajali ni dereva kushindwa kuchukua
tahadhari wakati akiendesha usiku na kuligonga trekta lililoegeshwa
barabarani.
Aliongeza kuwa, SUMATRA ime amu a k u s i t i s h a l e s
e n i za usafirishaji kwa mabasi yanayomilikiwa na kampuni hiyo katika
njia ya Moshi-Babati yenye namba za usajili T898 BKN, T267AZL na
T212BLZ.
Leseni za usafirishaji kwa magari hayo zitatolewa baada ya
kukamilisha maagizo kama yaliyotolewa kwenye kampuni ya Osaka Rolay
Class.
Bw. Mziray alisema Desemba 12 mwaka huu, basi la Kampuni ya
Burdani Bus Service, lenye namba T610 ATR likitokea Korogwe kwenda Dar
es Salaam, lilipata ajali Kijiji cha Taula, Wilaya ya Handeni na
kusababisha vifo vya watu 12, majeruhi 93.
Basi hilo lilikuwa
likiendeshwa na Bw. Ruta Kwadahel ambapo taarifa za jeshi zilisema
chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, uzembe wa dereva na kujaza abiria
kupita kiasi.
SUMATRA imechukua hatua ya kusitisha leseni za
usafirishaji kwa mabasi yanayomilikiwa na kampuni hiyo yenye namba
T158BXG, T610ATR, T572BXJ, T994AGD na T607ATR.
Leseni za usafirishaji kwa magari hayo zitatolewa baada ya kampuni hiyo kukamilisha maagizo waliyopewa wenzao
Chanzo;Majira
0 comments: