Baadhi ya wananchi wakilishuhudi Lori hilo likiinuliwa kutoka kwenye mtaro
Hatari wakati zoezi la kuliinua lori
hilo likiendelea watoto hao walinaswa na kamera za Mtandao huu waliingi
kwenye mtaro wakisaka mafuta ya Petroli yaliomwagika kutoka kwenye lori
hilo
Vibaka hao walitumia ngazi hizi kupanda juu ya Lori hili na kushusha mizigo iliyokuwa juu ya Tenk
Lori hilo baada ya kuinuliwa
Vijana hao wakitimu mbio baada ya kuona kamera za Mtandao huu zikiwamulika wakati wakizoa mafuta hayo.
NA DUSTAN SHEKIDELE,MOROGORO.
KATIKA hali ya kushangaza Lori la mafuta
aina ya Scania lenye namba za usajiri T772 BAZ limetumbukia lenye bila
dereva kwenye mtaro uliopo eneo la Kihonda barabara kuu ya Morogoro
Dodoma baada ya dereva wa Lori hilo kushuka na kuliacha gari hilo bila
kulizima na kuwafukuza wezi waliokuwa juu ya tenk la gari hilo
wakishusha mizigo.
Shuhuda wa tukio hilo Bw Joseph Furahisha alipohojiwa na mtandao huub alisema
" Dereva wa Lori hili alipofika pele
kwenye tuta alishuhudia pikipiki ikiwasha taa na kuzima aliamua
kuongeza umakini na kubani kwamba mmoja wa abiri aliyekuwa kwenye
pikipiki hiyo alipanda juu ya Tenk na kushusha maboksi ya Oil ndipo
dereva huyo aliposhuka fasta akajisahau kuvuta 'endbrack'hivyo wakati
akiwafukuza wezi hao huku Lori hilo lililokuwa kwenye mtelemko
lilitembea bila dereva na kuingia kwenye mtaro huu"alisema shuhuda huyo.
Dereva wa Lori hilo Bw ldd Hoza
alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alisema alikuwa akisafirisha
mafuta ya petroli kutoka Dar es salaama kueleka Dodoma na kwamba
alipofika kwenye daraja la Kihonda alipunguza mwendo kwa lengo la
kulipanda tuta lililokuwa eneo hilo la daraja.
" Kwa kawadi dereva unapopunguza mwendo
ni lazima uangalie kwenye kioo nyuma yako kuna nini hivyo nilipoangalia
niliona dereva wa pikipiki akiwasha taa na kuzima nilipochunguza zaidi
nikaona mtu yuko juu ya Tenk akishusha maboksi ya Oil nikashuka na
kumfukuza kwakuwa eneo hili ni la mtelemko gari hili ilitembea yenye na
kuingia kwenye mtaro na wezi hao walifanikiwa kuondoka na boksi moja la
oil kwa kutumia pikipiki yao"alisema Dereva huyo ambaye mpaka muda huu huyo hapo eneo la Tukio
Chanzo: Shekidele
0 comments: