Gari
ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Meck Sadicky likinasuliwa kwenye tope
baada ya kukwama katika kijiji cha Mataya-Ruvu Chini,yote hiyo ikiwa ni
sehemu ya changamoto ya Miundo mbinu hasa barabara,Wakati wakiongoza
msafara wa Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa
anakwenda kukagua chanzo cha Maji Ruvu chini na kujionea upanuzi wa
chanzo hicho mapema jana jioni;wakati Ndugu Kinana alipokuwa
akihimitimisha ziara yake ya siku tatu ndani ya wilaya ya
Kinondoni,ziara hiyo ikiwa na lengo la Kuimarisha uhai wa chama cha CCM
na kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu utekelezaji wa Ilani ya
uchaguzi 2010.
Utaratibu wa kulinasua ukiendelea.
OOppss..haya twendeeeee....!
Mkuu
wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh.Mecky Sadicky akimfafanulia jambo Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,mara baada ya kukumbana na changamoto ya
miundombinu,wakati wakielekea kukagua
chanzo cha Maji Ruvu chini na kujionea hali halisi na kazi kubwa
inayofanyika ya upanuzi wa chanzo hicho mapema jana jioni,wakati Ndugu
Kinana alipokuwa akihimitimisha ziara yake ya siku tatu ndani ya wilaya
ya Kinondoni,ziara hiyo ikiwa na lengo la Kuimarisha uhai wa chama cha
CCM na kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu utekelezaji wa Ilani ya
uchaguzi 2010.
Wakitafakari
namna ya kupita mara baada ya kukutana na changamoto ya
miundombinu,hasa barabara kama uonavyo pichani Lori likiwa limeziba njia
kutokana na hali ya mvua kunyesha eneo hilo.
0 comments: