Serikali ya Tanzania imesema kuwa imebaini kuwepo kwa
biashara haramu ya kusafirisha watoto wa kike kwenda nchini China kwa
lengo la kuwashirikisha katika ukahaba ambao unadaiwa kusababisha
kunyanyaswa kwa wasichana hao na wengine kuuawa.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa
kimatifa nchini humo Bernard Membe amesema serikali itatuma wachunguzi
nchini Uchina kuchunguza biashara hiyo.
Hatua hiyo imechukuliwa mwezi mmoja baada ya msichana mmoja Mtanzania kuuawa kikatili katika mji wa Guangzhou nchini Uchina.
Waziri Membe amesema huenda baadhi ya wahusika
wa bishara hiyo ni Watanzania wanaosafirisha wasichana wa dogo kwa
kisingizio cha kuwatafutia ajira. Baadhi ya wanaosafirishwa hujipata
pabaya baada ya kuwasili Uchina ambapo hunyang'anywa hati zao za usafiri
na kulazimishwa kushiriki ukahaba.
Baadhi ya wakaazi wa Dar es laam waliozungumza
na BBC wameelezea kusikitishwa na vitendo hivyo na kuitaka serikali
ichukue hatua.
0 comments: