m
Habari zilizotufikia hivi sasa zinasema kituo cha kuuzia mafuta cha Victoria petrol station kinaungua mda huu, habari za haraka inasemeka nyuma ya kituo hiko kuna moto unawaka na zimamoto washafika eneo la tukio kusaidia kuzima moto huo, habari kamili itakujia punde.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu kilichokuwa kikiwaka moto ni bohari la madawa mali ya kampuni ya Philips. Vitu vingine ni pamoja na jokofu la kuhifadhi vimeteketezwa kwa moto ambapo bado chanzo cha moto huo hakijafahamika bado
Bohari hilo lipo maeneo ya Kipanga Jet kuelekea Barabara ya Nyerere jirani na kituo cha mafuta cha Victoria.
Kwa ujumla moto huo umedhibitiwa na zaidi ya kuaharibu madawa hayo na thamani hakuna madhara makubwa yaliyotokea kwa bidanamu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wapo eneo la tukio ambako hali bado si shwari.
Sehemu iliyoathirika zaidi ni ghala la kutunzia dawa za binadamu la kampuni ya Philips.
0 comments: