HATARI! VIJANA WAJIRUSHA BAHARINI KUTOKA JUU YA PANTONI KWENYE KIVUKO CHA KIGAMBONI DAR

 Kijana alionekana anaruka kutoka Juu ya Pantoni (Kivuko) mbele kidogo baada ya Pantoni hiyo MV. Magogoni kuanza safari zake, huku abiria wengi wakiwa wameacha viti vyao na kuendelea kushangaa.
Wakati huo huo mwengine nae alionekana anachomokea kutoka katika Pantoni hiyo na kuzamia majini.
Wasafiri walipigwa butwaa zaidi kuona kasi ya vijana hao inazidi kuongezeka na huyu kijanda ndiye aliyekuwa anafunga dimba la kuzamia majini.
Ni zaidi ya Vijana 9 wote walipanda Pantoni ya MV. Magogoni bila ulinzi wowote na baadae kupiga mbizi wakitokea katika Pantoni hilo. 
PICHA ZOTE NA DAR ES SALAAM YETU 

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: