Chanzo: Bongo5
Waendesha
vyombo vya moto barabarani wamerahisishiwa njia ya kununua na kulipia
mafuta kwa njia ya M-Pesa, kufuatia ushirikiano kati ya kampuni ya simu
za mkononi Vodacom M-Pesa na kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta
ya Total Tanzania. Ushirikiano huo umeanzia kwenye vituo vichache vya
Total Tanzania na baadae kusambaa maeneo mbalimbali nchini, lengo kuu ni
kuhakikisha kila mtanzania anaemiliki chombo cha moto anakuwa na uwezo
wa kununua na kulipia mafuta kwa njia iliyo salama na
uhakika.
uhakika.
Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akiongea na waandishi
wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kulipia mafuta kwa Mpesa
kwenye vituo vya mafuta vya Total nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa
Biashara wa Total Romee de Villeneuve. Uzinduzi huo umefanyika leo
jijini Dra es salaam
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,
Salum Mwalim, amesema siku zote kampuni yake imekuwa msitari wa mbele
katika kurahisisha maisha ya Watanzania kupitia miundombinu ya
kiteknolojia iliyo nayo.
“Tumekuwa
tukibuni njia mbalimbali kila siku kwa lengo la kuwapa urahisi wateja
wetu na kuwaondolea adha ambazo wanaweza kuzipata wakiwa wanataka
kununua mafuta kutoka vituo vya Total Tanzania, sasa wateja wetu wote
kupita M-Pesa ambayo siku hizi imechukua nafasi kubwa sana katika mfumo
wa maisha ya binadamu wana uwezo wa kununua na kulipia mafuta kutoka
vituo ivyo vya mafuta,” alisema Mwalim.
Aidha,
Mwalim aliongeza kuwa kampuni ya Vodacom kupitia M-Pesa wataendelea
kuwaletea wateja mambo mengi ambayo hayajawahi kutokea nchini, lengo
likiwa ni kuhakikisha biashara zote nchini zimeunganishwa na M-Pesa ili
kwenda sambamba ambapo hadi sasa tayari biashara zaidi ya 320
zimeshaunganishwa na huduma hiyo.
“Tunatambua
watu wengi wanahitaji la kununua mafuta kwa ajili ya magari au piki
piki zao lakini kwa bahati mbaya wanaweza kufika kwenye kituo cha mafuta
wakiwa na fedha pungufu, sasa wasiwe na wasi wasi wowote endapo
watakuwa na fedha katika akaunti zao
za M-Pesa wanaweza kutatua tatizo hilo,” alisisitiza Mwalim.
za M-Pesa wanaweza kutatua tatizo hilo,” alisisitiza Mwalim.
Kwa
upande wake Meneja wa Maendeleo, Ubora na Mafunzo wa Kituo cha mafuta
cha Total Tanzania, Maria Lebby, Amesema kupitia njia hii wateja wa
Total watanufaika kutokana na namna kampuni hiyo ilivyo jidhatiti katika
kurahisisha njia za malipo.
“Tumekuwa
tukipokea wateja mbalimbali kwa nyakati tofauti zikiwemo za usiku
ambazo ni hatarishi kwa usalama wa fedha alizobeba mteja, hivyo basi
kuanzia sasa mteja wetu anaweza kutembea bila yakubeba fedha taslimu na
badala yake kuziweka kwenye akaunti yake ya M-Pesa na kujihakikishia
anapata huduma akiwa na amani juu ya usalama wa fedha zake.”
Aidha
Meneja huyo aliendelea kubainisha manufaa watakayopata wateja kwa
kusema “huu ni wakati wakutumia teknolojia tulizonazo ili kurahisisha
upatikanaji wa huduma kwa watanzania, waliowengi wanapenda kufanya mambo
yao kwa uharaka hasa wanapokuwa na majukumu mengine yakufanya, kupitia
huduma hii tatizo hilo litakuwa limetatuliwa. Natoa wito kwa makampuni
mengine kukubali kupokea mapinduzi yanayoletwa na teknolojia ili kuweza
kwenda na wakati na kurahisisha mfumo mzima wa upatikanaji wa huduma.”
<!--
0 comments: