Umeshawahi kusikia au kuona raia wanasimamisha gari la polisi linapokuwa patrol mitaani na kuomba kuweka pozi mbele ya gari na kupiga picha? Au wengine kuwaomba maaskari wawakamate kwa kosa lolote ili tu watoe nuksi kwa kupanda magari ya polisi ya kifahari wakati wanapelekwa kituoni? Basi hayo yanajiri Dubai.
Amini usiamini brand za magari zilizojaa katika garage ya polisi ya Dubai ni Lamborgini, McLaren MP4-12C, Aston Martin, Ferrari, Bentley na Chevrolet.
Mwaka jana tuliwahi kuandika kuhusu chuo cha Dubai ‘American University in Dubai’ chenye wanafunzi wengi wanaomiliki magari ya kifahari duniani, lakini sasa ni polisi wa Dubai ambao wamenunuliwa magari hayo kwaajili ya kufanya patrol za kawaida mitaani.
Hata maaskari wenyewe wa Dubai wamekiri kuchanganyikiwa baada ya kupewa magari hayo kwaajili ya kufanyia kazi.
Mmoja wa askari hao aitwaye Mariam Ahmed, ambaye binafsi anamiliki Toyota Land Cruiser amesema alipokabidhiwa kuendesha Ferrari FF kwaajili ya doria mitaani hakuamini, na huwa anatamani asipate Off awe kazini muda wote sababu ana enjoy kuwa kwenye Lamborgini awapo zamu.
“Ni mara yangu ya kwanza kuendesha Sport car”, alisema “waliponichagua sikuamini, ni raha sana kuiendesha, nikiwa off huwa naimiss sana siwezi kuifananisha na Land Cruiser yangu”.
Aliongeza, “inafurahisha sababu kuna watu huwa wanatuomba tuwakamate kwa sababu yoyote ya kubambikiza ili tu wapande Ferrari wakati wa kwenda polisi”.
Askari mwingine aitwaye Abdullah Mohammed , alisema magari hayo yamewaongezea ujiko wanapokuwa wanayaendesha mitaani.
“Kinachofurahisha zaidi katika kuendesha gari kama hiyo ya kifahari ni jinsi watu wanavyokutazama na tabasamu kubwa”.
Kwa mujibu wa GeeksTopten Dubai ndio inakamata nafasi ya kwanza katika Top 10 ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na magari ya polisi ya gharama zaidi 2014, ‘Top 10 Countries Having Most Expensive Police Cars in 2014’.
Tazama video za magari hayo na watu wakiyasimamisha ili wapige picha.
Source: Oddity Central
0 comments: