MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA) WAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Fadhili Manongi akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini (hawapo pichani) juu ya Kanuni na taratibu za Mamlaka hiyo katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Masuala ya Anga Julius Kamhabwa,Inspekta Mwanadamizi Idara ya Udhibiti wa Mamlaka ya Anga Tanzania Mutesigwa Mango(kushoto).
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari nchini na waadishi wa habari wakimsikiliza kwa makaini Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Fadhili Manongi (hayupo pichani) wakati alipokuwa akiwaelezea shughuli mbalimbali ,Kanuni na taratibu za Mamlaka hiyo wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Inspekta Mwanadamizi Idara ya udhibiti Maswala ya Anga,Mutesigwa Mango ,akifafanua jambo kuhusiana na ajira za Maarubani na wahudumu wa ndege hapa nchini wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo vya habari uliohusu kanuni na taratibu za Mamlaka hiyo,Mkuatano huo ulifanyika katika hoteli ya Peacoco jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Fadhili Manongi .Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Masuala ya Anga Julius Kamhabwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akifafanua jambo wakati alipohudhuria mkutano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ulioandaliwa mahususi kwa Wahariri wa Vyaombo vya habari jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia wanaomsikiliza ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Fadhili Manongi , Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Masuala ya Anga, Julius Kamhabwa.

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: