Foleni Dar: Mohammed Dewji apanda boda boda kuwahi mkutano, afikiria kununua helikopta!!

Foleni Dar: Mohammed Dewji apanda boda boda kuwahi mkutano, afikiria kununua helikopta!!Foleni ya magari Dar es Salaam huwa kali zaidi pale mvua zinaponyesha na si jambo la ajabu kutumia saa nzima kufika eneo ambalo kwa kawaida ungeweza kutumia dakika 5 tu.
Mbunge wa Singida Mjini,  Mohammed Dewji leo amejikuta katika wakati mgumu kutokana na foleni hiyo kali ya magari. Hata hivyo akili yake ilichemka haraka na kuamua kusahau kuwa alitajwa kwenye orodha ya Forbes 2013 ya watu matajiri zaidi Afrika, kukodi piki piki aka boda boda.
“The traffic in Dar is crazy,I was so fed up sitting in the car, I had to rent a(Boda Boda) 2 make it 4 a meeting, I guess I need a chopper,” alitweet.
Huenda wazo la kununua chopper akalifikiria kwa nafasi kubwa zaidi ili kuepukana na foleni kali wakati mwingine na hivyo kushindwa kuhudhuria mikutano ya maana.

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: