Katika
hatua nyingine, abiria 60 walikwama kusafiri jana kutoka Dar es Salaam
kwenda Bukoba, mkoani Kagera baada ya kudanganywa na mawakala bandia
katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo kwa kuuziwa tiketi feki.
Matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika kituo hicho
hususani katika msimu huu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, kutokana
na kuongezeka kwa idadi abiria wa kwenda mikoani.
Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti katika kituo hicho, abiria hao walisema kuwa walidanganywa na kukatiwa tiketi ya mabasi ambayo hayafanyi safari zake kwenda Bukoba jana baada ya kumaliza taratibu zote ikiwa ni pamoja na kulipa nauli.
“Sisi hatuwezi kujua kwa kuwa tiketi zote zilionekana sahihi, lakini tunashangaa leo (jana) kutuambia basi hilo haliendi tena Bukoba wakati kila kitu kilifanyika hadharani, tunahitaji msaada wa kusafiri,” alisema Rwegasira Muhingo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, Ofisa wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Polisi wa Kinondoni, Yusuph Kamotta, alisema watu watatu wamekamatwa kuhusiana na matukio kama hayo.
“Watuhumiwa hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi, tumefanya hivyo ili kuhakikisha abiria hao wanarudishiwa fedha zao,” alisema.
Komotta alisema abiria hao walikatiwa tiketi za basi la Nicatico baada ya mawakala hao kuwadanganya wakati wakijua basi halifanyi safari hiyo na kuwatoza nauli kati ya Sh. 60,000 hadi Sh.70,000.
Ofisa Leseni kutoka Sumatra, Sebastian Lohay, alitoa wito kwa wamiliki wa mabasi kuhakikisha wanahifadhi nyaraka zote za magari, zikiwamo tiketi na sare kwa baadhi ya wapiga debe ili wasizitumie kudanganya abiria.
Wakati huo huo, Lohay alibainisha kuwa Sumatra itachukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuyatoza faini magari yatakayokwenda kinyume cha masharti yao ya usajili likiwamo kuongeza nauli.
Imeandikwa na Isaya Kisimbilu, Miriam Mshana na Leonce Zimbandu.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments: