Kampuni
ya Transevents Marketing Ltd kutoka Nchini Tanzania kwa kushirikiana na
kampuni la Dutch Amfibious Transport(DAT) linalotengeneza mabasi ambayo
kutoka Uholanzi yanauwezo wa kutembea nchi kavu na majini na ambayo
itakuwa ni Teknolojia ya kwanza kwa Afrika itakayo anzia Tanzania kuwa
na aina hiyo ya mabasi.
Mabasi
hayo ya aina yake ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria wa kutosha
yanatarajiwa kuzinduliwa mwakani nchini Tanzania , pamoja na hayo mabasi
hayo yataweza kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa na kurahisisha swala
zima la usafiri ambapo mabasi hayo na baadhi ya magari mengine madogo
yatakuwa na uwezo wa kupita majini na Nchi kavu.
Baadhi ya Mabasi hayo yatakuwa yanatokea Mombasa hadi Mtwara kupitia Baharini kisha nchi kavu.
Mchakato huo umekwisha anza kufanyiwa kazi pia kwa ushirikiano wa SUMATRA
Mchakato huu umekwisha anza kufanyiwa upembuzi yakinifu na kazi pia kwa ushirikiano na taasisi pamoja na Mamlaka mbalimbali za hapa nchini zikiwemo, SUMATRA, Jeshi la Polisi na kitengo cha Usalama barabarani.
Mchakato huu umekwisha anza kufanyiwa upembuzi yakinifu na kazi pia kwa ushirikiano na taasisi pamoja na Mamlaka mbalimbali za hapa nchini zikiwemo, SUMATRA, Jeshi la Polisi na kitengo cha Usalama barabarani.
Video hizi Mbili zinaelezea kwa kina na kuonesha jinsi Mabasi haya yatakavyokuwa yakifanya kazi hapa nchini Tanzania
Tazama Video la Basi hilo tangia Linatengenezwa hadi Linafanyiwa majaribio
Tazama video ya Basi hilo Likiwa linafanya safari zake Nchi kavu na Baharini pamoja na abiria ndani.
0 comments: