Kutokana
na adha wanayopata abiria wanaofanya safari zao kati ya Kivukoni na
Mnazi Mmoja, SUMATRA ikishirikiana na kikosi cha usalama barabarani
(Kanda maalumu) imerudisha usafiri huo ambapo mabasi ya UDA sita (kwa
kuanzia) yatakuwa yanafanya safari kila siku katika maeneo hayo.
Usafiri
huu umeanza rasmi jana tarehe 12.02.2014 asubuhi, japo kulikuwa na
matatizo ya hapa na pale lakini kwa kuwa wote (SUMATRA, Polisi na UDA
tulikuwa barabarani tuliweza kurekebisha kasoro hizo kwa pamoja.
Njia zitakazotumika ni kama ifuatavyo:
Kutoka
Mnazi Mmoja: Zittanzia Mnazi Mmoja kisha zitakwenda hadi kituo cha
Baridi na kuendelea na safari kwa kutumia barabara ya Bibi Titi hadi
Maktaba kisha zitaingia kulia kwenda Posta Mpya na kwenda Ferry.
Kutoka
Kivukoni (Ferry): Yatatumia njia hizo bali zitakapofika makutano ya
barabara za Bibi Titi na Uhuru (Traffic light) zitaingia kulia hadi
makutano ya barabara za Uhuru na Lumumba kisha zitaingia kushoto hadi
eneo zilipoanzia safari kwa ajili ya kuchukua abiri akwenda Ferry.
Tunatarajia idadi ya mabasi itakuwa inaongezeka kuendana na mahitaji, na nakuli itakayotumia ni shilingi 400/= tu.
Conrad Shio
Afisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki
K. Shio
Kny: MKURUGENZI MKUU
0 comments: