Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimueleza jambo Mbunge wa jimbo
la Nkasi Kaskazini,Mh.Ali Mohammed Kessy,walipokuwa wakitembea kwa miguu
kufuatia msafara huo kukumbana na changamoto ya barabara mapema jana
jioni katikati ya Msitu wa hifadhi ya wilaya ya Nkasi.Ndugu Kinana na
Msafara wake ulikuwa umetoka kijiji cha Namanyere kuelekea kijiji cha
Mwampemba kusikiliza matatizo ya Wananchi na kukagua miradi mbalimbali
ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya mwaka
2010.
Barabara
hiyo yenye urefu wa kilometa 100,lakini iliwachukua zaidi ya masaa 12
kwenda na kurudi kutokana na ubovu wa barabara.Ndugu Kinana yuko Mkoani
Rukwa,Katavi na Kigoma kwa ziara ya siku 21 ya kuimarisha Chama cha
CCM,kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kiwemo na kuzisikiliza kero
mbalimbali za wananchi
Ndugu
Kinana akishiriki kuweka mawe sehemu korofi,angalau kusaidia Lori hilo
pichani lililolala ndani ya msitu huo kwa siku mbili,wapite nae msafara
wake uweze kuendelea na safari.
Sehemu
korofi ya Barabara ikiwekwa sawa ili lori lipite na kisha msafara nao
uweze kupita,lakini hata hivyo zilitumika juhudi kubwa kuvusha msafara
wa Kinana na hatimae kuendelea na safari ya kuelekea kijiji kingine.
Kila mmoja akipumua kivyake,baada ya kuvuka salama sehemu korofi ya barabara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (anaerusha jiwe) akishiriki kuziba sehemu korofi kwa mawe,ili msafara uweze kupita
Pichani
kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongoza kuvuka sehemu korofi
ya barabara kwa miguu,huku madereva wakipiga hesabu zao namna ya
kupita.PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-NKASI RUKWA.
0 comments: