Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya madereva na makondakta kupambana na abiria waliokuwa wakipinga nauli ya sh 1,300.
Akizungumza na wananchi pamoja na madereva jijini Dar es Salaam juzi, Ofisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki, Conrad Shio, alisema hakuna haja kwa madereva hao kuzua mgogoro wakati kila kitu kiko wazi.
Alisema Sumatra imeamua abiria watozwe nauli ya sh 750 baada ya kubaini umbali wanaosafiri hauzidi kilomita 25.5.
“Kama kuna dereva na kondakta asiyetaka kuwatoza abiria hao ni vema akaondoa gari lake katika barabara hiyo,” aliema Shio.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimbiji, Ubaya Abdallah, alisema madereva hao awali kabla kijiji hicho hakijaingizwa kwenye ramani ya Sumatra walikuwa wakitoza nauli sh 1,300.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments: