Mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda na wafanyabiashara, viwanda na kilimo Tanzania mkoa wa Iringa TCCI , Lucas Mwakabungu (katikati),akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya utafiti uliofanywa na Institute of Business Environment Strengtheniing for Tanzania (IMED) kwa kushirikiana na Tanzania Chamber of Commerce,Industries and Agriculture (TCCIA) Mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa mwanzoni mwa wiki.(Picha na Denis Mlowe)
======== ======= =========
Na Denis Mlowe,Iringa.
UTAFITI uliofanywa na Institute of Business Environment Strengtheniing for Tanzania (IMED) kwa kushirikiana na Tanzania Chamber of Commerce,Industries and Agriculture (TCCIA) Mkoa wa Iringa umebaini Tanzania inapoteza mapato zaidi ya shilingi bilioni 174 kwa mwaka kutokana na wakulima kutotumia mizani katika upimaji wa mazao ya mahindi na mpunga.
Mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda na wafanyabiashara, viwanda na kilimo Tanzania mkoa wa Iringa TCCI , Lucas Mwakabungu amebainisha hayo wakati akzungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa kuwa utafiti huo kuhusu sheria ya vipimo na mizani wa mwaka 1982 unavyosimamiwa na kutekelezwa na kurudiwa Julai na Septemba mwaka 2013.
Alisema utafiti huo unaonyesha kwa kiasi gani wakala wa vipimo na mizani unatekeleza sheria hiyo na wafabyabiashara na wakulima wanaifuata na kuitekeleza iadha madhara na matokeo ya kutoifuata sheria hiyo.
Mwakabungu alibainisha kuwa mikoa ya Iringa na Njombe pekee inapoteza ushuru wa mazao (crop Cess) ya mahindi na mpunga zaidi ya shilingi bilioni 2.5 kwa mwaka kutokana na mikoa hiyo kuhusika na kilimo cha mazao hayo. Alisema ushuru wa kodi ya mazao unaopotea kwa mazao ya mahindi na mpunga kwa nchi nzima kwa msimu ni shilingi bilioni 14.8.
Alisema utafiti uliofanywa na IMED ulichukua sampuli za magunia 43 ya mpunga yaliyopimwa uzito na wakala wa vipimo na mizani (WMA) kati ya magunia 482 yaliyokamatwa na kubainika kuwa uzito halisi wa kila gunia ulikuwa wa wastani wa kilo 42 zaidi ya uzito unaostahili sawa na asilimia 56.
Aidha alibainisha kuwa uzito wa wastani wa gunia la mahindi lililojazwa kwa ndoo za plastiki lina kilo 36 zaidi ya uzito unaostahili sawa na asilimia 40 kutokana na lumbesa ambayo wakulima wanadidimizwa na wafanyabiashara.
Alisema wakulima wanatumia ndoo za plastiki na lumbesa kwa kuwa kuna upungufu wa mizani na ushuru wa mazao kulipwa kwa gunia badala ya uzito na kutokuwepo kwa vifungishio vinavyokubalika.
Mwakabungu alisema utafiti huo ilibainisha kuwa wakala wa vipimo na mizani(WMA) hawana rasimali fedha za kutosha, vifaa vya kutosha na hawana rasimali watu wa kutosha kuwezesha kuitekeleza sheria hiyo kama inavyotakiwa.
0 comments: