CCM Mbeya wataka Serikali kuwapa Tazara Wachina

File:Tazara crossing bridge.jpgChama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya, kimependekeza Wachina wapewe madaraka ya kuendesha Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) kuondokana na kero, shida na matatizo yanayowakabili wafanyakazi wa shirika hilo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Godfrey Zambi alitoa pendekezo hilo wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuzungumza na wafanyakazi wa Tazara Mkoa wa Mbeya, jana.
Zambi alisema Tazara ina matatizo mengi, ikiwamo ya ufundi na hata ufisadi, na kwamba, njia pekee ya kuepukana nayo nikuwaruhusu Wachina waichukue reli hiyo kuiendesha.
Awali, wafanyakazi wa Tazara eneo la Tunduma hadi Makambaku walisoma risala yao ambayo ilitaja matatizo 10 yakiwamo ya kutopelekwa ufisadi.
Walisema licha ya kuzalisha fedha za kutosha , wanashindwa kuwalipa mishahara. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU) kanda hiyo, Christopher Kiziyo alisema licha ya Serikali kulipa malimbikizo ya mishahara, mshahara wa mwezi uliopita haujatoka hadi sasa. Naye msoma risala ya wafanyakazi, Shaaban Malekela alisema wanashangaa viongozi wa Tazara wanashindwa kusafirisha mafuta kwa reli, badala yake wanasafirisha kwa malori yanayoharibu barabara.
Chanzo: Mwananchi

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: