Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kimataifa wa nchi za bonde la ufa unaojadili miundombinu na uchukuzi kwa upande wa mashariki, kusini na Afrika ya kati, daktari Mwakyembe matumizi ya reli ndio njia mbadala ya kulinda ubora barabara na kusisitiza tatizo lililopo sekta binafsi inashindwa kuwekeza katika reli kutokana na kuhitaji gharama kubwa na idadi kubwa ya mabenki yanamasharti magumu.
Awali akielezea changamoto za uchukuzi katika ukanda wa kati,mtaalamu wa miundombinu kutoka mamlaka ya uwezeshaji wa uchukuzi kanda ya kati-TTFA- mhandisi Charles Sabiti ameainisha changamoto zinazoikabili sekta ya uchukuzi katika ukanda huo zikiwemo mfumo mbovu wa reli,kutokuwepo kwa viwango sawa vya vipimo vya uzito wa mizigo pamoja na ucheleweshwaji wa nyaraka sahihi za waingiza mizigo.
Kwa upande wake meneja mradi kutoka shirika la entico ambao ndio waandaji wa mkutano huo,bwana Warren Ersen amesema lengo la mkutano huo ni kuwawezesha washiriki kutoka zaidi ya nchi 12 kubadilishana uzoefu wa namna ya kukabiliana na changamoto za miundombinu na kuongeza na wawekezaji,ambapo amesisitiza hakuna uwezekano wa kuboresha sekta ya uchukuzi kwa kipindi kifupi na kusisitiza inachukua zaidi ya miaka 6 matokeo yake usaidia kushusha gharama za bidhaa kwa watumiaji kutokana na unafuu wa usafirishaji.
0 comments: