Ni muhimu kuzingatia vipimo unaponunua tairi za gari yako for a safe and comfortable drive.
Tairi zikitofautiana even a single dimension ni tatizo.
Tairi mbili za mbele na tairi mbili za nyuma au tairi zote lazima zilingane vipimo.
Namna ya kuangalia vipimo vya tairi :
Mfano tairi imeandikwa 205/70R14 au P 205/70R14 maana yake;
P = Passenger ie gari binafsi au ya abiria
205 = Upana wa tairi ni 205mm
70 = Urefu wa tairi ( kutoka ardhini hadi inapoanza rim) ni 70% ya Upana.
R = Muundo wa tairi ni Radial
14 = Diameter ya rim ni 14 inch.
Vipimo vinakuwa kwa mfumo kama ilivyo katika mfano huo hapo juu na vinaandikwa pembeni kwenye tairi.
Angalia mfano wa picha hapo chini.
0 comments: