Polisi mkoani, Tabora wamewahakikishia ulinzi na usalama wa
kutosha madereva na abiria wote wa magari yatakayotumia Barabara Kuu ya
Dar es Salaam-Mwanza kupitia Igunga na Nzega.
Akizungumza na Mwananchi jana, Kamanda wa Polisi
mkoani humo, Peter Ouma alisema barabara hiyo imekuwa na matukio mengi
ya utekaji wa magari ya mizigo na abiria.
Alisema kufuatia hali hiyo, polisi wamejipanga kukabiliana na majambazi wanaofanya vitendo hivyo.
Kauli hiyo imekuja baada ya magari matatu ya mizigo kutekwa na madereva wake kujeruhiwa vibaya.
Kitendo hicho kimesababisha mgomo mkubwa wa madereva na abiria wanahofia usalama wao na mali zao.
Kamanda huyo alisema tukio lililotokea juzi ni sawa matukio mengine ya uhalifu yanayofanywa na watu hao.
Alisema polisi wa doria wamejipanga ili kuhakikisha kuwa watekaji hao wanatiwa mbaroni na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, hatua hiyo itaambatana na kuimarishwa kwa usalama katika barabara mbalimbali mkoani Tabora.
“Ninawahakikishia madereva na abiria wote
wanaotumia barabara hizi kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa kwa usiku
na mchana naomba ushirikiano kutoka kwa wananchi,” alisema kamanda Ouma.
Alisema polisi wanafanya uchunguzi kuhusu askari
waliosababisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watachukuliwa hatua za
kinidhamu.
Kamanda Ouma aliwataka wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara kushirikiana na jeshi hilo kwa kufichua wahalifu.
Kuhusu mgomo alisema ulikwisha juzi jioni huku magari ya abiria yakipewa kipaumbele kuendelea na safari.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nzega Emmanueli Mihayo, alisema afya za majeruhi wa magari yaliyotekwa zinaendelea vizuri.
Chanzo;Mwananchi
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nzega Emmanueli Mihayo, alisema afya za majeruhi wa magari yaliyotekwa zinaendelea vizuri.
Chanzo;Mwananchi
0 comments: