Chanzo: Bongo5
Barabara kadhaa za katikati ya jiji la Johannesburg kuanzia leo Jumanne zitafungwa kupisha shooting ya filamu ya The Avengers.
Uchukuaji wa filamu hiyo utaanza saa 12 jioni hadi Jumatano asubuhi.
Mitaa
mingine itafungwa kuanzia February 14 hadi 23. Mitaa itakayoathirika ni
President Street kwenda Rissik na Eloff streets na Joubert Street
kwenda Harrison na Rissik streets. Polisi wamesema sehemu za mitaa ya
Commissioner, Sauer na Albetina Sisulu nayo itafungwa.
Muendelezo
wa filamu hiyo ya Hollywood, iliyopewa jina ‘Avengers: Age of Ultron’
utahusisha waigizaji maarufu wakiwemo Robert Downey Jr, Scarlett
Johansson, Chris Evans na Chris Hemsworth.
0 comments: