Mwezi
huu Facebook imetimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake na naweza
kudhubutu kusema kuwa mtandao huu umekuwa ni miongoni mwa mitandao
mikubwa na yenye mafanikio duniani
Mtandao
huu umefanikiwa kubadilisha kwa kiasi kikubwa utamaduni wetu wa kupanga
safari na kutembela maeneo mbalimbali, kwa ujumla naweza kusema
kumekuwa na mafanikio na madhara ambayo yameletwa kama mabadiliko katika
sekta ya usafiri nchini na dunia kote.
Mabadiliko yafuatayo yanaweza kueleza vizuri mchango wa facebook kwenye ulimwengu wa sasa wa usafiri.
Ndoto
za kusafiri zinaweza kutimia: Ukiingia tu kwenye facebook na kukutana
na picha za marafiki zako wakiwa wamepanda ndege (plane), farasi au basi au hata
bodaboda, au wakionyesha wako katika hifadhi za taifa ni rahisi mno
kwako wewe kuipata picha na kujiona tayari umeshafika eneo hilo, wakati
mwingine waweza hata kuona wivu kwanini haujafika eneo hilo au kwanini
mpenzi/mzazi/rafiki yako hajakupeleka huko.
Tunapata
taarifa nyingi: Kupitia makundi na kurasa za
marafiki na jamaa, ukiweka maswali yako yakiuliza ni wapi panafaa
kutembelea au wapi unafikiria kutembelea wakati wa mapumziko au sikukuu
basi marafiki watachangia mawazo na kukupa maelezo mengi tu, jambo
linalokufanya usiku na mchana uendelee kuota ndoto za mahala hapo.
wataaalmu wanasema kuwa kadri unavyokuwa na mawazo chanya juu ya kitu
unachokipanga, furaha huongezeka na kukifanya kitu hicho kutoakea kweli.
Ushauri kutoka kwa marafiki zetu: Unapoweka nia yako ya
kutaka kusafiri kwenda mahala na kutaka kupata maoni ya rafiki zako, kwa
mfano "hoteli gani ni nzuri kwa familia mkoani Morogoro" hapa kila mtu
atachangia kulingana na uzoefu wake na weledi na mwisho wa siku utapata
ushauri utakaokusaidia katika safari yako.
Ukweli kwa haraka: Zamani ilikuwa ngumu kidogo ililazimika siku, miezi
na pengine miaka ndio uweze ku-share uzoefu wako katika safari au
kuonyesha ndugu jamaa na marafiki picha zako ulizopiga ukiwa kwenye
matembezi fulani, lakini sasa mtu yuko mbugani anaweza kupiga picha na
kuiweka facebook na marafiki zake kujionea kinachoendelea.
Kujua
ulipo: Huu unaweza kuwa ni uzuri lakini unaweza kuwa ubaya pia wa
facebook, maana unaponesha uko eneo fulani wakati mwingine inaweza
kufichua jambo ambalo hukutaka lijulikane, mfano mzuri umetoroka
nyumbani na kwenda na marafiki zao pahala na mkapiga picha na wenzako
kuweka kwenye facebook, kuna hatari ya wazazi au ndugu, walimu au walezi
kuona picha hizo na baadae kukushikisha adabu
Huondoa
upweke: Japokuwa kwa sasa facebook kama inapoteza umaarufu wake lakini
imekuwa iki-play great role katika kuondoa msongo wa mawazo na upweke,
jambo ambalo mtu anaweza kuwasiliana na watu wengine na kubadilishana
mawazo hata kama yuko mbali na familia akiwa safarini.
Safari moja, kwa pamoja
0 comments: