UBAYA WA GARI NI HUU

KONDA NA DEREVA  HOI HADI MADOGO WAME INGILIA KATI Ikiwa ni tatizo la ubovu wa miundombinu katika jiji la Dar es Salaam kumepelekea makonda na madeleva kuwa katika hali ngumu katika baadhi ya maeneo.
Kutokana na tatizo la barabara limepelekea kuchelewa kwa kufika katika vituo kwa haraka ili abiria waweze kuelekea kwenye majukumu yao ya kila siku.
Dereva na Konda baaada ya kumuona mwandishi BK walieleza malalamiko yao juu ya barabara za uswazi zilivyosahulika.
“Dahh maeneo mengi ya barabara za uswahilini yapo ovyo sana so inatuchukua muda mrefu kufika stand sehemu ya kwenda kwa nusu saa mtu unatumia takribani masaa 4, so tunaomba serikali iyangalie na barabara za uswahilini ambazo zinasaidia kupunguza jam kwenye barabara kuu, pamoja na hivyo boss anadai chake kwa hali hii itakuwa ugomvi kila siku na mabosi wetu.”
Uswahili kumesahulika serikali inaombwa kuzikarabati barabara ili kuondokana na adha hizi za foleni.

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: