Vijana wa Bodaboda wakiwa katika picha ya pamoja na diwaniwa wa kata ya
Kingo Fidelis Tailo baada ya kukabidhiwa pikipiki 8 walizonunuliana
kutokana na michango yao.
Habari zaidi soma hapa
DIWANI wa kata ya Kingo katika manispaa ya Morogoro
Fidelis Tairo amewataka vijana wa
Bodaboda kuepuka kufanya matukio ya uharifu na badala yake wawe walizni wa watu
wanaofanya uharifu.
Alisema hayo jana
wakati akikabidhi pikipiki 8 za kikundi cha Nunge bodaboda zenye thamani ya
shilingi milioni 13.2 zilizonunuliwa na vijana hao kutokana na michango yao.
Alisema kumekuwa na dhana
kuwa bodaboda wengi ni waporaji na waharifu na kwamba dhana hiyo ni vema
wakaifuta ili kujenga uaminifu kwa wateja wao.
‘’ Mimi kama diwani wa kata hii nisingependa kukuta kijana
wangu amejitumbukiza katika matukio ya kiarifu, fanyeni kazi za uhalali’’
Alisema.
Alisema serikali ya
chama cha Mapinduzi inatambua umuhimu wa biashara ya usafiri wa bodaboda
na ndio maana imewaondolea kodi kwa lengo
la kuwafanya vijana wengi kuweza kujiajiri na kuepuka tabia ya kukaa
vijiweni bila kazi hali inayosababisha kuingia katika makundi yasiofaa.
Kwa upande wake katibu wa kikundi hicho Dickson Paskari
alisema mafanikio hayo waliyapata baada ya kukaa na kubuni kitu cha kufanya ili
kuweza kujiajiri wenyewe na kupata kipato kinachotesheleza.
‘’ Tulianza kwa kuchanga kiasi cha shilingi 6000 kila siku
kwa watu 8 na kila mwezi tuakawa
tunanunua pikipiki moja tunampatia mmoja anaanza kazi’’ Alisema
Alisema awali
walipoanza vijana wenzao waliwabeza kuona kuwa hawatafanikiwa na kwamba
waliongeza juhudi ili kuhakikisha nia yao haiishii njiani.
Alisema kwa sasa wanampango wa kusajiri kikundi chao ili
kuweza kufanya shughuli za kiuchumi zaidi na kwamba lengo ni kusaidiana katika
kujikwamua kiuchumi.
0 comments: