Takriban watu 300 wakiwa bado
hawajapatikana, siku moja baada ya ajali, ripoti za ujumbe wa simu
uliotumwa na wale waliokuwa wamekwama ndani ya meli hiyo zimeibuka
kupitia vyombo vya habari nchini humo.
Mwanafunzi:"huenda hii ndio
mara yangu ya mwisho kukuambia kuwa nakupenda,'' ndio ulikuwa ujumbe wa
mwanafunzi mmoja kwa jina Shin Young-Jin kwa mamake.
Kulingana na jarida la Herald nchini humo, Shin alikuwa miongoni mwa watu 179 waliookolewa.
Lakini wazazi wengine waliopokea ujumbe kama huo bado hawajaweza kupatana na watoto wao.
Mwanafunzi: "baba usijali, nimevaa boya la kujiokoa na niko na wasichana wenzangu. Tuko ndani ya meli na bado hatujaanza kuokolewa.''
Baba: Najua msaada uko njiani , lakini kwa nini hamjaanza kuelea, tafadhali jaribu kuondoka ndani ya meli kama unaweza.''
Mwanafunzi: ''Kuna msongamano mkubwa na meli tayari imeanza kuzama''
Mwanafunzi aliyetuma ujumbe huu bado hajapatikana.
Familia za abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo walijawa na hisia wakisubiri taarifa zozote kuhusu wapendwa wao.
Mwanafunzi: "meli imekwama na haisongi walinzi wa baharini wameanza kuwasili kujua hitilafu imetokana na nini'
Kakake:'' usiwe na wasiwasi. Fanya kila mnachoamrishwa kufanya na kila kitu kitakuwa shwari.''
Lakini hapakuwa na mawasiliano mengine baada ya hapo.
Baadhi ya wazazi waliweza kuendelea kuwasiliana na watoto wao, hadi mawasiliano yalipokatika.
0 comments: