ZIJUE NJIA ZAIDI YA 60 ZA DALADALA DAR ZINAZOSITISHWA NA SERIKALI

Njia 64 za magari ya daladala jijini Dar es Salaam zitakoma kutumika kutokana na kuanza kwa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART).
Kwa kuanzia matayarisho ya kupisha mradi huo, Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (DART) umetaka wamiliki wote wa mabasi ya daladala yanayopita katika Barabara ya Morogoro au kukatiza katika njia hiyo, kufika katika ofisi zake kujiandikisha.  

Mhandisi wa Wakala , John Shauri aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa wamiliki hao wanatakiwa kufika katika ofisi za DART zilizoko jengo la Ubungo Plaza barabara ya Morogoro kuanzia leo hadi Aprili 21 mwaka huu kwa ajili ya kujiandikisha kama moja ya matayarisho ya kupisha mradi huo.

DART iko kwenye mchakato wa kuwezesha upatikanaji wa watoa huduma kwenye mfumo mpya wa mabasi yaendayo haraka awamu ya kwanza ambayo inajumuisha barabara ya Morogoro, Kawawa na Mtaa wa Msimbazi kwa njia kuu na nyingine za kiungo.

Alisema kulingana na mpango wa uendeshaji wa mfumo wa DART, barabara zinazohusika zitapaswa kutumiwa na mabasi ya mfumo huo pekee.

Shauri alitaja baadhi ya njia zitakazoguswa na ni pamoja na Mbagala Rangi 3 kwenda Masaki, Vingunguti kwenda Makumbusho, Kunduchi Kwenda Mwenge, na Msata kwenda Ubungo.

Njia nyingine ni Kariakoo kwenda Makumbusho, Buguruni kwenda Kawe, Kivukoni kwenda Mburahati, Mbagala Kuu kwenda Mwenge, na Mkata kwenda Ubungo. Njia nyingine ni Mburahati kwenda Muhimbili, Segerea kwenda Mwenge, Vingunguti kwenda Kawe, Vingunguti kwenda Mbezi, Kunduchi kwenda Posta, na Kunduchi kwenda Makumbusho.  

Pia alitaja Temeke kwenda Masaki, Kivukoni kwenda Mabibo, Muhimbili kwenda Mabibo, Posta kwenda Ubungo, Posta kwenda Mabibo, Kawe kwenda Kimara, Kivukoni kwenda Mbezi, Mwenge kwenda Mbezi, Posta kwenda Mbezi, Mbezi kwenda Tegeta na Bunju kwenda Makumbusho.

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

1 comment:

  1. No deposit casino bonuses - DrmCD
    › no-deposit-casino 용인 출장안마 › no-deposit-casino 동해 출장샵 You can find 대전광역 출장안마 a list of no deposit casino bonus offers in 거제 출장샵 the UK. All the best no deposit casino bonus offers from the 진주 출장샵 UK. Deposit bonuses can

    ReplyDelete