Shughuli za uchukuzi wa mizigo toka
bandarini kwenda mikoani na nchi za jirani kwa njia ya reli ya Tazara
zitasimama kwa siku saba,kufuatia maji ya mvua zinazoendelea kunyesha
jijini Dar-es-Salaam,kusomba tuta la reli ya tazara umbali wa mita
arobaini na kuacha mataruma ya reli hiyo yakining'inia.
Meneja mkuu wa mkoa wa mamalaka ya reli ya Tanzania
na Zambia Tazara, mhandisi Abdalah Kimweri amesema kuwa mvua
zinazoendelea kunyesha jijini Dar-es-Salaam,zimeathiri miundombinu ya
mamlaka hiyo umbali wa kilometa nane kati ya maeneo ya kurasini na yombo
jijini Dar-es-Salaam.
Mhandisi huyo medai kuwa,katika maeneo mengi
inapopita reli hiyo hasa jijini Dar-es-Salaam,makambako mkoani njome na
tunduma jijini mbeya baadhi ya wananchi wamejenga karibu kabisa na reli
hiyo jambo ambalo ni hatari kwao na kwa reli ya Tazara na kudai kuwa
tayari wameisha wajulisha wananchi kuondoa maendeleo yao kabla ya hatua
kali za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.
Mhandisi ujenzi wa mamlaka hiyo ya Tazara kwa
upande wa Tanzania mhandisi Richard Festo,amesema kuwa katika maeneo ya
temeke jijini Dar-es-salaam,ujenzi holela wa mfumo wa mitaro kuelekezewa
kupita kwenye njia ya reli kumechangi kwa kiasi kikubwa kuchangia
kuharibu miundombinu ya mamlaka hiyo,huku baadhi ya wananchi wakitaka
kulipwa fidia kwa makaburi yao yaliyosombwa na maji.
Reli ya tazara yenye historia ya urafiki baina ya
nchi tatu za Tanzania ,Zambia na uchina ikiwa na urefu wa kilometa 1860
kutoka jijini Dar-es-salaam nchini Tanzania hadi new kaplimposhi nchini
Zambia ,iliyoanza kutumika kusafirisha abiria na mizigo kwenye mikoa ya
Pwani,Morogoro,Iringa na Mbeya iliyo anza kutoa huduma hiyo mwanzaoni
mwa miaka ya 1976 ikiwa imejengwa na kampuni kutoka China.
0 comments: