Mh. Lowasa ashiriki tamasha la waendesha bodaboda mkoa wa Dar es Salaam

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwahutubia Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambapo Mh. Lowassa alikuwa ni Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyofana sana.

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza machache kwenye Tamasha hilo kabla ya Kumkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Tamasha hiloKamanda wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga akizungumza akitoa hotuba yake mbele ya Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
 
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Mfuko wa PSPF kwa kutoa Mchambo mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael Roewe akisoma Risala yao mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Afisa mwandamizi wa fedha wa PSPF, Hidaya Mganga akimsaidia kujaza fomu mmoja wa waendesha bodaboda aliyejitokeza kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari wa PSPF

Wakati tamasha hilo likiendelea waendesha bodaboda wengi walifurika kwenye banda la mfuko wa pensheni wa PSPF kujisajili na kujiunga na mpango wa hiari wa uchangiaji PSS.
Afisa wa mpango wa hiari Mwajuma Ali akipitia fomu za usajili wakati wa tamasha hilo
Afisa wa uendeshaji PSPF, Halima Isaa akiwaelekeza namna ya kujaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS
Mtumishi wa PSPF akigawa vipeperushi kwa waendesha bodaboda vinavyoeleza namna ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari

Afisa fedha wa PSPF, Reginald Msafiri akigawa vipeperushi







Msanii Linex akifanya yake Viwanjani hapo mapema leo.
Mh. Lowasa akiwaaga waendesha bodaboda

Watumishi wa PSPF katika picha ya pamoja

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: