Picha: RC Njombe akwama kwenye tope barabara ya Makete

Gari la mkuu wa mkoa wa Njombe likiwa limekwama kwenye tope kijiji cha utweve makete. 
 Wadau wakisukuma gari hilo, na huyu ni mwenyekiti wa kijiji cha Utweve akijitahidi kusukuma.
 Hali tete hapa, gari hilo likiwa limenasa mtaroni
 wadau wakijitahidi kuvuta gari hilo
 jitihada zikiendelea.
Gari la mkuu wa mkoa wa Njombe, kapteni mstaafu Aseri Msangi limekwama kwa zaidi ya saa kadhaa katika kijiji cha Utweve wilayani Makete wakati akiwa ziarani kukagua maendeleo ya sekondari ya wasichana makete inayojengwa kijijini hapo

Adha hiyo ilimkumba mkuu wa mkoa baada ya mvua kubwa kunyesha wakati akifanya mkutano na wananchi shuleni hapo mara baada ya kuikagua shule hiyo na kuridhishwa na jinsi ilivyojengwa

Mtandao huu wa eddy blog umeshuhudia magari mengine yaliyokuwa yametangulia gari la mkuu wa mkoa yakipita eneo hilo lililokuwa na utelezi mwingi huku gari hilo la mkuu wa mkoa likikwama kutokana na utelezi huo

Jitihada za kulinasua gari hilo zilifanywa na msafara mzima ulioambatana na mkuu wa mkoa pamoja na wananchi wa kijiji hicho ambapo zoezi hilo lilichukua zaidi ya saa moja kutokana na mvua kuzidi kunyesha zaidi

Jitihada hizo zilizaa matunda na hatimaye gari hilo lilinasuliwa na mkuu wa mkoa kuendelea na safari yake, na hakuna madhara yoyote yaliyotokea

HABARI/PICHA NA EDDY BLOG

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: