Na Bakari Masasi (MUM)
Wafanyakazi
wa kampuni ya Strabag, inayojenga barabara ya mabasi yaendayo kasi,
wakimdhibiti kijana aliyetuhumiwa kuiba vifaa vya ujenzi wa miundombinu
ya barabara na kukwamisha kwa muda maendeleo ya ujenzi huo katika eneo
la Magomeni Kagera jijini Dar es salaam.
Hata
hivyo, kundi la vijana wanaodhaniwa kuwa vibaka wenziye, walifanikiwa
kumkomboa kijana huyo kabla ya kufikishwa kwenye mikono ya sheria, baada
ya kutokea tafrani kubwa kati ya wahuni hao na wafanyakazi wa Strabag
waliopewa dhamana ya ujenzi huo na serikali ya Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania, chini ya wizara ya ujenzi inayoongozwa na Mh. Magufuri.
Katika
tukio hilo, mmoja wa wafanyakazi wa Strabag (aliyemshika kijana huyo,
Pichani) alijeruhiwa vibaya kwa mawe kutoka kwa wahuni hao wakati wa
harakati hizo za kumkomboa mwenzao ambaye walitokomea naye vichochoroni
huku bado akiwa amefungwa kamba.
0 comments: