Wakimbizi 98 wazama ziwa Albert uganda

Umoja wa Mataifa umesema kuwa takriban watu 98, wamekufa maji baada ya boti walimokuwa wanasafiria kuzama wiki jana katika Ziwa Albert Magharibi mwa Uganda.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, limesema kuwa watu 41 wameokolewa na wengine wengi bado hawajapatikana.
Boti hiyo ilikuwa imewabeba wakimbizi wa DRC waliokuwa wanarejea makwao kutoka katika kambi ya wakimbizi nchini Uganda.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa umewarejesha manusura nchini Uganda ambako wanapokea msaada.

BBC

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: