Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne Mcintosh,
akizungumza na Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi
wa Mercedes Benz Afrika katika mpango mkakati wa kubadilishana nao
mawazo na uzoefu katika shughuli za biashara na masoko katika ukanda wa
Afrika.
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes
Benz ukanda wa Afrika ni kutembelea kampuni hiyo kubwa na ya siku
nyingi ya magari hapa duniani na kuangalia aina mpya za bidhaa ambazo
zipo sokoni na kupata kujifunza kazi mbalimbali za kijamii ambazo
kampuni hiyo ya CFAO Motors inafanya hapa Tanzania.
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes
Benz Afrika kutoka nchi za Rwanda, Sudan, Afrika Kusini na nchi zingine
wamekuja nchi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na wamefanikiwa
kujifunza shughuli mbalimbali za ufundi na utendaji kazi wa kampuni ya
CFAO Tanzania.
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes
Benz Afrika pia walipata fursa ya kuangali akarakana ya kampuni hiyo
kwenye maeneo ya Vingunguti na kuona shughuli za ufundi kwa magari yao
ambapo wateja ambao wanaharibikiwa na magari wanaweza kupata huduma hiyo
kwenye karakana ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors, Charles-Edouard CAMBOURNAC
akitoa maelezo kwa Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na
Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika.
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes
Benz Afrika wakitembelea eneo linalotoa huduma ya kutengeneza kwa
teknolojia ya hali ya juu magari ya wateja wa kampuni hiyo pindi
yanapopata hitilafu.
Baadhi ya magari ya wateja wa Kampuni ya CFAO Motors yakisubiri kuhudumiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors, Wayne Mcintosh (katikati)
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors,
Charles-Edouard CAMBOURNAC, wakati wa Ziara ya kujifunza kutoka Wakuu wa
Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika.
Kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed.
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes
Benz Afrika wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufika makao makuu
ya kampuni hiyo.
Baadhi ya kikundi cha wamasai walioburudisha Wakuu wa Mercedes
Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika kwa kucheza
ngoma za Kimasai.
Baadhi ya Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi
wa Mercedes Benz Afrika wakichukua kumbukumbu za matukio kwenye simu zao
wakati kikundi cha Kimasai kilipokuwa kinatoa burudani.
Meneja Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed akifurahi jambo na mmoja wajumbe hao.
0 comments: