News Alert: Meli ya mizigo yazama ziwa Victoria

Meli ya mizigo iliyokuwa inatoka Bukoba kwenda Mwanza, ikiwa na wafanyakazi kumi na shehena ya sukari, imezama ziwa victoria katikati ya visiwa vya Kerebe na Bumbile. 

Chanzo EATV
read more →

MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA TAREHE 28/04/2014. TRAFFIC CIRCULATION AT CBD

Key: 1. RANGI YA NJANO - Njia ya Uelekeo Mmoja {One Way}.
 2. RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya Mielekeo Miwili {Two Way} 
 3. RANGI YA KIJANI - Mitaa ya Kutembea kwa Miguu Magari marufuku {Walking Streets} 
 4. RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita Daladala
 5. RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART
 6. DUARA ZA NJANO - Mzunguuko {Roundabout} 
 7. MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye Taa za kuongozea Magari {Singnalized Intersection}
1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower Magari  kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument. 

2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi Makutano ya Mtaa wa Maktaba Posta Ya Zamani Magari yatakuwa yanaelekea Uelekeo mmoja wa Station Posta ya Zamani tofauti na ilivyo sasa Posta ya Zamani kwenda Station. 

3. Barabara ya Kivukoni  Kuanzia Posta ya Zamani hadi Ferry itakuwa barabara ya mielekeo miwili (Two Ways).

4. Barabara ya Samora kuanzia Mnara wa Askari hadi Ocean Road Hospitali itakuwa ni barabara ya mielekeo miwili.

5. Daladala Zote zitakazotokea barabara za  Makataba zitakunja kulia pembeni ya Jengo la NBC na hadi Makutano ya Mkwepu na kukunja kushito kuingia Sokoine pale Posta ya Zamani na baadaye kukunja kushoto kuingia Makataba na kurudi Posta Mpya .

Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Ofisi za DART
UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA.
AU.
OFISI YA MHANDISI WA MANISPAA YA ILALA
MABALA NA SHOPRITE SUPEEMARKET JIRANK NA KAMATA

Mtaarifu mwingine juu ya mabadiliko haya kuondoa usumbufu ifikapo siku ya Jumatatu 28/04/2014. PASAKA NJEMA
read more →

Inasikitisha: Soma ujumbe wa mwisho wa wanafunzi kwa wazazi dakika chache kabla ya meli kuzama

Ujumbe wa mwanafunzi mmoja kwa mamake wakati meli ilipokuwa inazama
Takriban watu 300 wakiwa bado hawajapatikana, siku moja baada ya ajali, ripoti za ujumbe wa simu uliotumwa na wale waliokuwa wamekwama ndani ya meli hiyo zimeibuka kupitia vyombo vya habari nchini humo.
Mwanafunzi:"huenda hii ndio mara yangu ya mwisho kukuambia kuwa nakupenda,'' ndio ulikuwa ujumbe wa mwanafunzi mmoja kwa jina Shin Young-Jin kwa mamake.
Mama:"na mimi nakupenda mwanangu,'' alijibu mamake Shin kwa ujumbe wa simu, bila kujua kilichokuwa kinaendelea.
Kulingana na jarida la Herald nchini humo, Shin alikuwa miongoni mwa watu 179 waliookolewa.
Lakini wazazi wengine waliopokea ujumbe kama huo bado hawajaweza kupatana na watoto wao.
Baadhi ya wazazi hawajaweza kuwapata watoto wao
Mawasiliano mengine kati ya mwanafunzi mmoja na babake , yalinukuliwa na shirika la habari la AFP.
Mwanafunzi: "baba usijali, nimevaa boya la kujiokoa na niko na wasichana wenzangu. Tuko ndani ya meli na bado hatujaanza kuokolewa.''
Baba: Najua msaada uko njiani , lakini kwa nini hamjaanza kuelea, tafadhali jaribu kuondoka ndani ya meli kama unaweza.''
Mwanafunzi: ''Kuna msongamano mkubwa na meli tayari imeanza kuzama''
Mwanafunzi aliyetuma ujumbe huu bado hajapatikana.
Familia za abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo walijawa na hisia wakisubiri taarifa zozote kuhusu wapendwa wao.
Abiria walishauriwa kutulia wakisubiri msaada
Katika ujumbe mwingine wa simu, mwanafuzni mmoja alimtumia ujumbe kakake mkubwa meli ilipoanza kuzama.
Mwanafunzi: "meli imekwama na haisongi walinzi wa baharini wameanza kuwasili kujua hitilafu imetokana na nini'
Kakake:'' usiwe na wasiwasi. Fanya kila mnachoamrishwa kufanya na kila kitu kitakuwa shwari.''
Lakini hapakuwa na mawasiliano mengine baada ya hapo.
Baadhi ya wazazi waliweza kuendelea kuwasiliana na watoto wao, hadi mawasiliano yalipokatika.
read more →

BODABODA MORO WAJA NA MBINU MPYA YA KUJIAJIRI WENYEWE

Vijana wa Bodaboda wakiwa katika picha ya pamoja na diwaniwa  wa kata ya Kingo Fidelis  Tailo baada ya kukabidhiwa pikipiki 8 walizonunuliana kutokana na michango yao.


Habari zaidi soma hapa


DIWANI wa kata ya Kingo katika manispaa ya Morogoro Fidelis  Tairo amewataka vijana wa Bodaboda kuepuka kufanya matukio ya uharifu na badala yake wawe walizni wa watu wanaofanya uharifu.

Alisema hayo  jana wakati akikabidhi pikipiki 8 za kikundi cha Nunge bodaboda zenye thamani ya shilingi milioni 13.2 zilizonunuliwa na vijana hao kutokana na michango yao.

Alisema kumekuwa na dhana  kuwa bodaboda wengi ni waporaji na waharifu na kwamba dhana hiyo ni vema wakaifuta ili kujenga uaminifu kwa wateja wao.

‘’ Mimi kama diwani wa kata hii nisingependa kukuta kijana wangu amejitumbukiza katika matukio ya kiarifu, fanyeni kazi za uhalali’’ Alisema.

Alisema serikali ya  chama cha Mapinduzi inatambua umuhimu wa biashara ya usafiri wa bodaboda na ndio maana imewaondolea kodi kwa lengo  la kuwafanya vijana wengi kuweza kujiajiri na kuepuka tabia ya kukaa vijiweni bila kazi hali inayosababisha kuingia katika makundi yasiofaa.

Kwa upande wake katibu wa kikundi hicho Dickson Paskari alisema mafanikio hayo waliyapata baada ya kukaa na kubuni kitu cha kufanya ili kuweza kujiajiri wenyewe na kupata kipato kinachotesheleza.

‘’ Tulianza kwa kuchanga kiasi cha shilingi 6000 kila siku kwa watu 8 na kila  mwezi tuakawa tunanunua pikipiki moja tunampatia mmoja anaanza kazi’’ Alisema

Alisema awali  walipoanza vijana wenzao waliwabeza kuona kuwa hawatafanikiwa na kwamba waliongeza juhudi ili kuhakikisha nia yao haiishii njiani.

Alisema kwa sasa wanampango wa kusajiri kikundi chao ili kuweza kufanya shughuli za kiuchumi zaidi na kwamba lengo ni kusaidiana katika kujikwamua kiuchumi.
read more →

Picha: Tazama mabasi mapya ya SUPER FEO, moto wa kuotea mbali

Ushindani wa kampuni za mabasi unazidi kuongezeka kwa makampuni hayo kuagiza mabasi mampya kila kukicha, tazama picha za mabasi matano mapya ya kampuni nya super feo aina ya YUTONG NEW MODEL







            Wanyama watano wa super feo wakiandaliwa kwa ajili ya kwenda nyumbani songea




                                                     Muonekano wa ndani wa super feo mpya






read more →

Meli iliyobeba watu 460 yazama huko Korea.K

Ferry yenye abiria 460 ikizama Korea Kusini.

Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za dharura zilizoripotiwa kutoka meli moja iliyobeba takriban abiria 460 katika pwani ya Korea Kusini.

Maafisa wanasema kuwa walinzi wa pwani hiyo wanatumia, meli za wanamaji wa Korea pamoja na ndege za uokoaji kuwaokoa watu waliokuwa katika meli hiyo.
Shughuli zinaendelea hivi sasa kuokoa zaidi ya abiria 460 wa ferry hiyo .
Jeshi la wanamaji likishirikiana na maafisa wanaolinda usalama katika bahari ya rasi ya Korea wanasema watu wengi wamefanikiwa kuolewa.

Maafisa wanasema walipokea habari kuwa meli hiyo imepata matatizo ikiwa imebeba idadi kubwa ya wanafunzi ikitoka Incheon iliyoko kwenye visiwa vya kifahari vya Jeju .
Waokoaji wamewanusuru tayari abiria 160 huku wengine waliosalia wakishauriwa waruke baharini iliwaokolewe.

Walioshuhudia wanasema kulisikika kishindo kikubwa kabla ya ferry hiyo kuanza kuzama zaidi ya kilomita 20 kutoka ufukweni.

Shughuli ya uokoaji bado inaendelea.

BBC/Swahili
read more →