News Alert: Basi la Zuberi lapata ajali laua wanne papo hapo – Singida

ajali-singida1
Picha hii haihusiki na ajali ya basi la Zuberi iliyotokea mchana huu huko wilayani Ikungi.
Mwandishi wetu, Ikungi
BASI la Zuberi lenye namba T119 AA2 limepata ajali mbaya katika kijiji cha Nkuhi wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida na watu wanne wameripotiwa kufa papo hapo kwa kukatwa vichwa huku majeruhi wengi wakiwa wameumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili.
Akizungumza na MOblog kutoka eneo la tukio leo mchana huu, mwandishi wa habari, Nathanieli Limu  amesema basi hilo la Zuberi lilikuwa linatoka Mwanza kuja Dar na lilikuwa na zaidi ya abiria 60.
Amesema kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa basi hilo alikuwa anajaribu kumkwepa bibi kizee aliyekuwa anakatisha barabarani kwenye majira ya saa saba mchana.
“ilikuwa si ajali ya kawaida baada ya bibi kizee kukatiza barabarani na wakati dereva anajaribu kumkwepa alirudi mara ya pili barabarani ndipo hapo gari lilipinduka na kuanguka kwenye mtaro,” amesema Limu
Alilisitiza kwamba mashuhuda wa ajali hiyo wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikiana baada ya bibi huyo kuamua kurudi mara ya pili barabarani na kusababisha ajali na kukaa kwa muda mrefu eneo la tukio.
Amesema kwa basi hilo la Zuberi liliinuliwa na lori lenye kifaa maalumu cha winch baada ya basi hilo kumlalia mtoto mdogo wa miezi kadhaa ambaye mama yake ni miongoni mwa waliofariki dunia papo hapo na maiti yake kupelekwa hospitali ya mkoa wa Singida.

Chanzo: Mo blog

Author

Written by DK

Napenda kusafiri, hasa kutembelea kila mkoa katika nchi yangu nzuri Tanzania, nafanya hivyo maana hiyo ndio njia niliyochukua katika kutumikia taaluma yangu ya habari na mawasiliano ya umma

0 comments: